Waliokamatwa na vipande vya meno ya Tembo 600 wafikishwa kortini

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Habari wanaJF,

Watuhumiwa 10 waliokamatwa na vipande 600 vya Meno ya tembo vyenye thamani ya shilingi Bilioni 4 wafikishwa Mahakama ya Kisutu.
 
WATU 10 wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwa kuratibu mtandoa wa ujangili unaojihusisha na usafirishaji wa meno ya tembo,

Watuhumiwa hao ni pamoja Ally Sharif (28), aliyekuwa akiishi Tabata Segerea, Raia wa Gunea; Victory Mawalla (29) Mkazi wa Kimara; Calist Mawalla (22) Mkazi wa Kibamba; Haruna Kassa (37) Mkazi wa Mwanangati.

Wengine ni Abbasi Jabu (40); Mkazi wa Mwanangati; Solomon Mtenya (46), Mkazi wa Kimara; Mussa Ligagabile, Mkazi wa Mbagala; Fatoumata Saumaolo (34) aliyekuwa akiishi Tabata Segerea, pia Raia wa Gunea; Khalfan Kahengele, Mkazi wa Keko na Ismail Kassa, Mkazi wa Kipunguni ‘B’.

Akiwasoma mashtaka hayo Paul Kadushi mbele Yohona Yongola Hakimu Katika Mahakama hiyo amedai kuwa, watuhumiwa hao wanashitakiwa kwa makosa matatu pamoja na kuhusika katika mtandao wa uharifu.

Kadushi amedai kuwa, kati ya tarehe 6 Aprili na 23 Machi mwaka huu watuhumiwa hao walipanga na kuratibu ununuzi na usafirishaji wa nyara za serikali ambazo ni meno 660 yenye thamani ya Sh.4.5 bilioni.

Shitaka la pili ni kujihusisha na usafirishaji wa nyara za serikali bila ya kibali cha maofisa wa wanyama pori ambapo walitenda hayo tarehe 6 Aprili na 23 Machi mwaka huu.

Wakati kesi hiyo ikiendelea

Shitaka la tatu linawahusu watuhumiwa watano pekee ambao ni Ally Sharif, Victory Mawalla, Calist Mawalla, Haruna Kassa, Abbasi Jabu ambao wanatuhumiwa kwa kosa la kukutwa na nyara za serikali ambazo meno ya tembo 660 yenye thamani ya Sh.4.5 bilioni.

Hakimu Yongola amesema kuwa, mahakam haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo na kwamba, watuhumiwa hao wahakuweza kujibu shauri hilo

Upelelezi huo haujakamilika hivyo shauri hilo litatajwa tena tarehe 28 Julai mwaka huu watuhumiwa wote wamerudishwa lumande .
 
Hawa ni watu wa kutumwa tu, angalia wengi
WanaWanakoishi hawa ni wa kutumwa tu, hili tatizo la tembo litaendelea kutusumbua kama mapapaa hawatakamatwa, meno 660 sio kitu ya kubeza, ingebidi uchunguzi uende mbali ili kujua nani anawatuma.
Kama una akili timamu unakubalije kutumwa kutanya uhalifu? Haya sasa ndo madhara yake.
 
Hayo meno tembo yameshakamatwa wahusika wangapi wameshachukuliwa hatua za kisheria mpaka sasa?tunasikia tuu wanakamatwa kinachoendelea hatujui
 
wakipandishwa kizimbani kesi imeisha husikii tena kinachoendelea ushahidi mnao mnasubiri nini? bongo utasikia meno ya Tembo yakapimwe kwa Mkemia kwanza...
 
Hili kosa kama sikosei ni la kuhujumu Uchumi, kwa vile Mahakama ya Ufisadi na Uhujumu Uchumi imeanzishwa kesi ipelekwe huko ili haki itendeke mara moja
 
Back
Top Bottom