Waliohamia CCM wote kutoswa uchaguzi mkuu 2020

Chifyono

JF-Expert Member
Oct 16, 2017
921
1,658
Habari wakuu
Kumekuwa na wimbi kubwa la wanachama wa vyama vya upinzani hususani chadema act na cuf kuwacha nyazifa zao za ubunge, udiwani na nafasi zingine ndani ya vyama vyao na kujiunga na chama cha ccm kwa sababu tu za kuunga juhudi za meko.

Ni vema ninyi mnaohama mkatambua, hakika mtakuja kulia na kujuta kwa maamuzi mnayoyachukua
Kwa sasa habari zinazojadiliwa ndani ya CCM ni kuona namna gani chama kinarudisha thaman yake kwa wanachama asilia.

Wanachama asilia wamecharuka kwa sababu wageni wamefika na kuwapora nafasi na teuzi mbalimbali

Hivyo ccm kimepanga hakuna kanjanja yeyote aliyehama upinzani na kujiunga CCM atapewa nafasi ya uongozi katika uchaguzi ujao.
 
Na walikuwepo watatoswa wengi tu, safari hii CCM wenyewe wataipata. Mtu kama Kangi Lugola, hivi CCM watawezaje kumsafisha kwenye campaign wananchi wamsamehe ili arudi tena bungeni?
 
Wakiruhusiwa kugombea tutakuwa tumeenda kinyume na katiba ya chama…..
 
Kwani mikataba yao inasemaje?
Malipo ya hela kwa muda wote uliobaki na kupewa nafasi ya kugombea tena kupitia Chama walichohamia bila kura za maoni ambapo lazima washinde hata kama wakishindwa.
 
Malipo ya hela kwa muda wote uliobaki na kupewa nafasi ya kugombea tena kupitia Chama walichohamia bila kura za maoni ambapo lazima washinde hata kama wakishindwa.
Ni kweli Mkuu, huku kwetu diwani alihama kutoka chadema mwaka 2018 akahamia ccm, wakati wa mchakato wa kupitisha majina kwa ajili ya kumpata mgombea wao kwa ajili ya uchaguzi uliokuwa unafuata palitokea mtifuano mkubwa, mpaka ikapelekea baadhi ya wajumbe waliokuwa wanapinga huyo mhamiaji kupewa nafasi kugombea tena wazuiwe kuingia kwenye kikao cha kamati iliyokuwa inafanya mchakato huo na kulazimisha apitishwe huyo mhamiaji kwa sababu kulikuwa na maelekezo kutoka kwa mwenyekiti wao wa taifa
 
Hawa watu wanajua uozo walionao ndo maana hata mikutano ya kisiasa wanaogopa kuiruhusu, siku wakifungulia milango, watararuriwa kiasi watakachojidharau kwa nn wanaendekeza biashara hii haramu!Ipo siku ushenzi huu utakoma nchini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom