kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,288
- 12,579
Mwl. Nyerere alikuwa miongoni mwa vijana wanufaika wakuu wa Utawala wa Wakoloni. Alipata nafasi ya kusomeshwa hadi vyuo vikuu na alikuwa ana ajira kwenye serikali ya wakoloni na kupata mshahara. Hawa ndio waliopaswa kuunga juhudi kwelikweli za utawala wa mkoloni.
Uhuru wetu huenda ungechelewa sana kama akina Mzee Nyerere R.I.P wangekubali kuondoka TANU na kwenda kuunga juhudi za Governor katika kuwasomesha watoto wa machifu na kuwapatia ajira za kudumu.
Leo hii wako vijana ambao walipiganiwa kwa jasho na damu za wananchi wenzao wanaotafuta mabadiliko kwa njia za maumivu makubwa dhidi ya chama tawala ambao waliwasaliti wananchi hao na kurudi CCM kwa kisingizio cha kwenda kuunga juhudi hata kabla jasho, damu na majeraha ya walioumizwa wakati wa uchaguzi hayajakauka na kupona.
Sasa ni wakati wa chaguzi tena, hawa vijana hawako tena upande ule uliowafanya wajulikane, wako upande ule unaolalamikiwa na wapinzani kwa mambo mengi. Bahati mbaya wengi wa vijana hawa hawakukubalika mbele ya wajumbe wa chama tawala walikohamia, na hawana uhakakika kwamba wasiowapenda ni wajumbe tu au hata wana CCM na wanchi kwa ujumla.
Je, vijana hawa wanalifahamu kosa lao?
Je, vijana hawa wanaujuwa ukubwa wa kosa lao?
Je, vijana hawa wanajutia kosa lao au walichokipata wakati wa kuunga juhudi hakiwafanyi wajutie?