kati ya vitu vilivyonifurahisha kuliko vyote jana ni kusikia zenji wamepigwa chini. wakubali tu kuwa wao sio nchi hata mataifa mengine yanajua hilo.
ZANZIBAR KUVULIWA UANACHAMA CAF NI BISHARA NJEMA
Maswali yamekuwa mengi sana bila ya majibu, suala kubwa kwa nini Zanzibar ilipewa uanachama CAF? ukianza kuzitazama sheria kwa nini nchi inapewa uanachama mchakato mzima mpaka hatua ya upigaji kura utaona kama miujiza.
Hili si jambo la bahati mbaya Mungu amelileta kwa makusudi yake. Vyovyote mtu atakavoliona kuwa kubwa au dogo, linaumuhimu au halina, kuwa zito au jepesi kwangu nimelitafsiri kuwa lina maana pana kwa mustakbali wa Zanzibar.
Kubadilika kwa mwanaadamu hakutokani na jambo kubwa sana mfano; afe mzazi wake au kutokee vita kwenye nchi yake laa si hayo tu kwanza lazima tujue kuwa kabadilika kwa binaadamu kunataka sababu ndogo tu ambayo Mungu ameshataka kumbadilisha mja wake.
Wakati mwengine huwa tunasema mtu fulani kabadilika kwa jambo la "kipuuzi" tu naam tunaliona kuwa ni la kipuuzi lakini Mungu ametaka hiyo ndio iwe sababu ya kumuongoa mja wake amtakae. Mimi si muumini wa Visasi, Kebehi, Kejeli na tambo za KIBURI naipigania HAKI, naitetea haki, lakini kwa njia zile zile za haki.
Kwa imani kabisa naamini kama madogo (ukiyaacha makubwa yalio/yanayo isibu Zanzibar) yaliweza kuwaweka watu karibu wakaweka udugu wa kitaifa kwanza na tukafanikiwa kuvuka kizingiti kikubwa basi sina wasi wasi kwa moyo wenye imani, kupitia njia za amani na hili linalooneka kuwa ni dogo ukilinganisha na mengi yenye kumbukumbu mbaya yanayoendelea kusemwa huenda hapa ndipo ilipo heri ya mabadiliko.
Mwisho tuweke hakiba kwa kurejea tena hizi sio zama za visasi na nongwa tukaishia kubezana na kuchukiana. Mungu anakadari zake anaweza kuyaleta mabadiliko kwa kumtumia kuku hayawan aso na akili