Waliodhoofisha media nchini hawa hapa

Waliodhoofisha media nchini hawa hapa

Nsimbi

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2014
Posts
1,091
Reaction score
1,204
Kwa sasa wahariri wengi wa vyombo vya habari hasa magazeti, wapo mifukoni mwa mafisadi.

Katika miaka ya 90 na mwanzoni mwa 2000s kulikuwa na magazeti na wahariri walitoa mchango mkubwa sana kuihabarisha jamii na kuibua uozo na kashfa kubwakubwa ndani ya Serikali na wafanyabiasha wakubwa kwa ujasiri mkubwa.

Baadae miaka ilivyozidi kwenda moto ule ukaanza kupungua makali yake na wahariri kugawanyika vipandevipande.

Why? Kwa sababu media ilianza kuingiliwa na wenye fedha hasa wafanyabiasha waliogundua njia nzuri ya kuwanyamazisha wanahabari ujasiri ni kuwatia 'mfukoni' .... Penyeza rupia... oops....hapo wahariri wanahabari wazalendo kabisa wakalegea kabisa kama mlenda!!

Kwa kweli kwa sasa suala la vibrance na upendo kwa nchi miongoni mwa wahariri wengi limebaki kuwa ni historia.

Hivi sasa wahariri wengi wanawatumikia wafanyabiasha na wanasiasa sio jamii.

WAFANYABIASHARA ndio wamechangia sana kuiua media na kuifanya ibakie kama a tooth less dog! Ama joka la kibisa! Baadhi ya hao mabwanyenye ni Rostam Aziz na vibaraka wake.

Kundi la pili lililoharibu ujasiri wa editors ni wanasiasa. From both CCM na Chadema wamewagawa sana wanahabari.

Hivi sasa habari zinaandikwa kwa kutegemea chama au mwanasiasa gani anatoa dau kubwa. Rushwa imetawala baadhi ya magazeti.

Mtu kama Lowassa amechangia sana kupooza ukali wa baadhi ya wahariri kwa kutumia fedha na ushawishi wake kuwahonga.

Kwa baadhi ya wahariri waandamizi, Lowassa ni "infallible figure"!! Mtagundua kuwa ni wanasiasa mafisadi ndio huwa wana tabia ya ku attempt kuwarubuni wanahabari kwa kutumia vihela vyao.

Wahariri wengi wenye 'mafanikio' ni wale waliojenga 'urafiki' na wanaotuhumiwa kuwa mafisadi kama niliotaja.

Kundi lingine lililochakachua ubora wa wahariri ni baadhi ya wakuu wa vyombo vya mashirika ya umma. Nani asiyejua kuwa wamewahonga sana jamaa hawa ili labda kufunika uozo mbali mbali. Baadhi yao ni Dk Dau? ama Erio? au Irene wa SSRA.

Kundi jingine lililoleta utepetevu katika magazeti na media kwa ujumla ni Serikali.

Hivi sasa State limeleta hofu na perplexity ndani newsrooms.
Sheria zilizotungwa hapa katikati zinadaiwa kukandamiza uhuru wa habari. Ni Serikali ya 'waoga' isiyotaka kukosolewa. Wanataka kusifiwa tu.

Mbinu za baadhi ya wanahabari kutaka kuchukua alternative ya kujipendekeza kwa rais haijafanikiwa kwani wa sasa haingiliki, hahongeki.

JPM huyu ndiye ambaye wakati anachukua fomu ya kugombea urais hakuna journalist aliyehongwa kama ilivyotokea wakati 'safari ya matumaini' ikizinduliwa kule Arusha.
Kweli mkamia maji... hayanywi!!!
 
Serikali no chanzo kikuu cha habari. Sheria zilizopitishwa kwa lengo la kudhibiti maudhui yanayoifikia jamii zimeharibu uhuru wa kujieleza, na haki ya kupata habari.
Siku hizi hakuna sababu ya kununua gazeti, au kukaa kuangalia taarifa ya habari. Kwa nini upoteze muda wako kuangalia taarifa za kumsifia mtu mmoja tu, au serikali ambayo tunajua imeundwa na wanadamu ambao hufanya makosa? Kwa nini taarifa zinazohusu ukosoaji hazirushwi au kuandikwa? Kwa maoni yangu, serikali imechangia kiasi kikubwa kuharibu uhuru wa habari. Hao mafisadi na watu wenye fedha wana mchango wao pia, lakini wangeweza kudhibitiwa kama kungekuwepo uhuru wa kujieleza
Unakumbuka kipindi kile Rostam yuko kwenye kitovu cha siasa za Tanzania? Gazeti la mwanahalisi lilimdhibiti na mambo yake anayofanya gizani yakajulikana. Hata akina Devidi Jairo bin jeuri ya rushwa walidhibitiwa.
 
Kwa sasa wahariri wengi wa vyombo vya habari hasa magazeti, wapo mifukoni mwa mafisadi.

Katika miaka ya 90 na mwanzoni mwa 2000s kulikuwa na magazeti na wahariri walitoa mchango mkubwa sana kuihabarisha jamii na kuibua uozo na kashfa kubwakubwa ndani ya Serikali na wafanyabiasha wakubwa kwa ujasiri mkubwa.

Baadae miaka ilivyozidi kwenda moto ule ukaanza kupungua makali yake na wahariri kugawanyika vipandevipande.

Why? Kwa sababu media ilianza kuingiliwa na wenye fedha hasa wafanyabiasha waliogundua njia nzuri ya kuwanyamazisha wanahabari ujasiri ni kuwatia 'mfukoni' .... Penyeza rupia... oops....hapo wahariri wanahabari wazalendo kabisa wakalegea kabisa kama mlenda!!

Kwa kweli kwa sasa suala la vibrance na upendo kwa nchi miongoni mwa wahariri wengi limebaki kuwa ni historia.

Hivi sasa wahariri wengi wanawatumikia wafanyabiasha na wanasiasa sio jamii.

WAFANYABIASHARA ndio wamechangia sana kuiua media na kuifanya ibakie kama a tooth less dog! Ama joka la kibisa! Baadhi ya hao mabwanyenye ni Rostam Aziz na vibaraka wake.

Kundi la pili lililoharibu ujasiri wa editors ni wanasiasa. From both CCM na Chadema wamewagawa sana wanahabari.

Hivi sasa habari zinaandikwa kwa kutegemea chama au mwanasiasa gani anatoa dau kubwa. Rushwa imetawala baadhi ya magazeti.

Mtu kama Lowassa amechangia sana kupooza ukali wa baadhi ya wahariri kwa kutumia fedha na ushawishi wake kuwahonga.

Kwa baadhi ya wahariri waandamizi, Lowassa ni "infallible figure"!! Mtagundua kuwa ni wanasiasa mafisadi ndio huwa wana tabia ya ku attempt kuwarubuni wanahabari kwa kutumia vihela vyao.

Wahariri wengi wenye 'mafanikio' ni wale waliojenga 'urafiki' na wanaotuhumiwa kuwa mafisadi kama niliotaja.

Kundi lingine lililochakachua ubora wa wahariri ni baadhi ya wakuu wa vyombo vya mashirika ya umma. Nani asiyejua kuwa wamewahonga sana jamaa hawa ili labda kufunika uozo mbali mbali. Baadhi yao ni Dk Dau? ama Erio? au Irene wa SSRA.

Kundi jingine lililoleta utepetevu katika magazeti na media kwa ujumla ni Serikali.

Hivi sasa State limeleta hofu na perplexity ndani newsrooms.
Sheria zilizotungwa hapa katikati zinadaiwa kukandamiza uhuru wa habari. Ni Serikali ya 'waoga' isiyotaka kukosolewa. Wanataka kusifiwa tu.

Mbinu za baadhi ya wanahabari kutaka kuchukua alternative ya kujipendekeza kwa rais haijafanikiwa kwani wa sasa haingiliki, hahongeki.

JPM huyu ndiye ambaye wakati anachukua fomu ya kugombea urais hakuna journalist aliyehongwa kama ilivyotokea wakati 'safari ya matumaini' ikizinduliwa kule Arusha.
Kweli mkamia maji... hayanywi!!!
Mkuu Nsimbi ulichoongea ni sahihi kabisa. Ila ukiondoa sababu binafsi za kwa nini waliingia kwenye fani, Ubangaizaji ni chanzo kikuu cha kudumaa kwa media.

Kama utakumbuka, baada ya mabadiliko ya kisiasa miaka ya 90, waanzilishi wengi wa media house, walikuwa ni wale waliokuwa na bifu binafsi na Mwl Nyerere. Hawakuwa na ajenda mbadala zaidi ya kufurahia Uhuru wasioujua.

Ni kutokana na hilo, hata ndani ya media House kuna vituko vingi kiasi kwamba, no serious and committed journalist atavumilia hivyo vituko. Angalia ni Waandishi wangapi wanaondoka.
 
Walioharibu media ni wanahabari wenyewe. Asinyooshewe kidole mtu yeyote. Wanahabari wanajua kwamba habari ni nini. Wanajua pia vipi watapata habari. Aidha wanajua waandike habari gani kwa kundi lipi. Wamefunzwa na kuaswa kuwa wakweli. Akitokea mtu akaenda kinyum ha haya, wa kulaumiwa ni mwandishi wa habari mwenyewe na si vingine. Wanahabari wanapaswa kuamka kutoka usingizini na kuwajibika ipasavyo. Jamii inahitaji habari na sio uhusiano na jamii (public relations).
 
Haliyeweka sheria kandamizi kwa wahariri ndio wa kwanza kuharibu vyombo vya habari nchini,lkn serikari ingeweka sheria rafiki kwa wana habari mambo yangekuwa vzr, serikari iangarie upya hili jambo.
 
NA NDIO KWA MWENDO HUU HUU, TUTAIUA JF
 
Kuna changamoto kubwa kurudisha heshima ya wahariri wa media nchini. Tuna vi editors corrupt kwelikweli. Ni kweli wa kulaumiwa ni wanahabari wenyewe lakini mafisadi wana mchango mkubwa kuitepetesha press kwa kutumia vihela vyao vya wizi.
 
umeleta mada ya ukweli mkuu,nchi imepoteza kabisa wale waandishi wa habari za kiuchunguzi,magazeti ya siku hizi ni ya kufungia vitumbua tu,ninakumbuka waandishi makini pale gazeti la mfanyakazi(hili gazeti lilikuwa linatoka kila jumamosi ila habari zake makini na zenye uhakika na ukweli,ilikuwa ikifika saa 6mchana hulioni tena mitaani ,sold out .
 
Fact mkuu, zile mambo za "makala moto moto" hakuna kabisa siku hizi.
 
Kuna changamoto kubwa kurudisha heshima ya wahariri wa media nchini. Tuna vi editors corrupt kwelikweli. Ni kweli wa kulaumiwa ni wanahabari wenyewe lakini mafisadi wana mchango mkubwa kuitepetesha press kwa kutumia vihela vyao vya wizi.
Ni sawa mkuu ila mimi najiuliza, hivi hao matajiri wanapotoa hivyo vijihela wanalazimisha? Si waandishi wanachukua kwa kukiuka maadili ya uandishi wa habari? Kuna taaluma unapoinmgia ni lazima ujitayarishe na yanayoweza kutokea. Mfano ni huu wa taaluma ya uandishi wa habari. wale wanaoingia humo kwa kudhani kuna pepo wamekosea sana. Aidha itakuwa jambo la ajabu mtu anajiunga na jeshi halafu anaogopa kufa vitani. Si asijiunge tu? Tunamuheshimu sana Jerry Muro, tunamkumbuka sana Mwaibabile na wengine.Hivyo ndivyo waandishi wanavyotakiwa wawe. Vinginevyo wamekosea njia
 
And What happened to Jery Muro the brave journalist is but history.
 
Rostam Aziz na Lowasa,Mwanahalisi la kipindi hiko na Raia mwema wanawajua.
 
Back
Top Bottom