Waliodai Yesu anakuja wafungwa miaka minne

Keykey

JF-Expert Member
Dec 1, 2006
3,250
740
Hawa jamaa kama kweli wana imani, ... ya Mungu wamwachie Mungu na ya Kaisari wampe Kaisari

Waliodai Yesu anakuja wafungwa miaka minne
:: Waliwatorosha watoto wa shule wakampokee Bwana

na ahmed makongo, bunda

MAHAKAMA ya Wilaya ya Bunda mkoani Mara, imewahukumu Wasabato wawili wenye msimamo mkali, kifungo cha miaka minne jela, baada ya kukiri kosa la kuwatorosha wanafunzi watatu wa shule ya msingi ili wamsubiri Yesu.

Wasabato hao, katika mahubiri yao, walisema Yesu angeshuka wakati wowote mwezi huu kutoka mbinguni.

Waliopewa adhabu hiyo iliyotolewa na Hakimu Mwandamizi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Richard Maganga, ni Lameck Masaka (45) na

Akisa Mbula (40); wote wakazi wa Kijiji cha Kiagata, Musoma Vijijini.

Hakimu Maganga alisema kuwa kutokana na kukiri makosa, kila mshitakiwa atatumikia kifungo cha miaka miwili jela.

Awali, ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Inspekta Edward Manoni, kuwa kati ya Machi 2 na 8, mwaka huu, washitakiwa ambao ni wazazi wa wanafunzi hao, waliwatorosha na kuwapeleka Kiagata, ambako walidai kwamba wanamsubiri Yesu ambaye angeshuka kijijini hapo. Inspekta Manoni alisema kuwa washitakiwa hao walifanya kosa hilo la kuwarubuni watoto na kuacha masomo kinyume cha sheria, huku wakijua kuwa kufanya hivyo ni kosa kubwa, kwani wanawanyima watoto haki yao ya msingi ya kupata elimu.

Washitakiwa wanadaiwa kuwa ni sehemu ya waumini wenye msimamo mkali waliojiengua kutoka kwenye Kanisa halisi.

Baada ya kuanzisha kanisa lao, waliweka kambi katika Kijiji cha Kiagata, kwa madai kuwa wanamsubiri YesuKristo.

Baadhi ya waumini waliuza vitu vyao, huku wanafunzi wakikataa kusoma kwa madai kuwa hakuna haja ya kusoma wakati ufalme wa Mungu umekwisha wadia.

Kambi ya Wasabato hao ilivunjwa na polisi kutokana na agizo la Serikali mkoani Mara.

Hii ni mara ya pili kwa Mahakama ya Wilaya ya Bunda, kuhumu Wasabato wanaodaiwa kuwa wenye msimamo mkali kwa makosa ya kutorosha wanafunzi.

Katika shauri la awali, wanawake wawili walihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka minne jela.

MTANZANIA
 
Ukisikia manabii wa uongo waliotabiriwa ndio hao. Hata hiyo miaka nne walohukumiwa naona midogo.
 
Hii si mara ya kwanza Matukio kama haya kutokea duniani.

Hata katika kuanzishwa kwa ADVENTIST MOVEMENT(SABATO) kule marekani na mkulima mmoja aitwaye William Miller watua pia waliuza vitu wakaenda kumsubili Yesu mlimani aje mara ya pili.

William Miller kabla ya kuwa mkiristo wa madhehebu ya BAPTIST alikuwa mtu wa kawaida tena haamini nguvu za Mungu(Deist)= a person who believes that God created the universe but has not been actively involved since).

NAYE ALITABIRI MIEZI KAMA HIYO HIYO(TRH 21 MARCH 1843 HADI TRH 21 MARCH 1844) KAMA WALIVYOTABIRI WATU WA MBEYA KUWA YESU ANARUDI MARCH 31 MWAKA HUU.

soma hapa www.religioustolerance.org/sda.htm
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom