Walioanzisha CCJ wafukuzwe Uongozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walioanzisha CCJ wafukuzwe Uongozi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OgwaluMapesa, Jun 2, 2011.

 1. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2011
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  UTAWALA wa Rais Jakaya Kikwete umekumbwa na misukosuko mingi, lakini zimekuwepo fursa kadhaa ambazo kama angezitumia vema zingeleta unafuu katika utawala wake.

  Wakati wa sakata la mkataba wa Richmond lililosababisha aliyekuwa waziri mkuu wake Edward Lowassa kujiuzuru na hivyo kuvunja baraza zima za mawaziri, ilikuwa ni fursa adimu kwa Kikwete kubadili sura na muundo wa baraza lake ili kujipanga upya.


  Yako makosa makubwa alikuwa ameyafanya wakati anaunda baraza hilo mwaka 2006 na angeweza kuyafanyia marekebisho baada ya Lowassa kujiuzuru na kuvunjika kwa baraza lile. Alishindwa.

  Ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe ilimpa fursa ya kufanyia mabadiliko baraza lake. Angeweza kuitumia ripoti ile, hata ambayo hayakuwamo katika mapendekezo ya ripoti.


  Alishauriwa vibaya. Akaipiga danadana na kupoteza fursa. Angeweza kuondokana na baadhi ya watendaji wakuu wa vyombo vya dola ambao wana uadilifu na utendaji unaotiliwa shaka, hata bila lawama kubwa kuelekezwa kwake kwa kuwa yeye hapendi lawama. Alishindwa kabisa kutumuia fursa hiyo.

  Zilifuata fursa nyingine ikiwamo ile ya wizi wa mabilioni ya shilingi katika akaunti ya madeni ya nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Angeondokana na watendaji au wanasiasa wenye utata wa mwonekano mbele ya jamii.

  Angeweza, bila ajizi, kutumia fursa zile nakufanya mabadiliko ya sura na muundo na kwa njia hiyo, angefanikiwa kuboresha utendaji na hatimaye rekodi yake binafsi katika kufanya maamuzi magumu. Alishindwa. Hivyo alizama zaidi katika tope la ufisadi; kuonekana anawaogopa mafisadi au anashiriki ufisadi.


  Fursa nyingine pana ilikuwa ni uchaguzi mkuu ambao ulimpa uwanja mpana kupitia kura za maoni na hata uteuzi baada ya uchaguzi. Wengi tulio na mapenzi na urais wa Kikwete tulisubiri kwa hamu kuona akitekeleza ahadi zake kadhaa alizotupa faraghani kuwa angetumia fursa hiyo kuondokana na wanachama na watendaji walio mzigo kwa chama na serikali.


  Tulishikwa na butwaa baada ya kuona akishindwa kabisa kuwafunga magoli mafisadi, wakati hata golikipa alikuwa ameondoka langoni. Kikwete siyo tu alipigana kidete kuona mafisadi wanapitishwa na vikao alivyoviongoza ili kugombea nafasi zao, bali pia alienda majimboni kuwaombea kura kwa wananchi bila aibu wala kigugumizi.


  Rais Kikwete aliwafokea na kuwakejeli waliodiriki kumwambia hatari au ubaya wa watu hao na walio wengi wakaufyata huku wakiacha mambo yaende kama alivyotaka. Hapa alishindwa pia kutumia fursa ya uchaguzi mkuu kuondokana na mafisadi aliokuwa anadai katika hotuba zake kuwa wanakifanya chama kionekane vibaya mbele ya wapigakura.


  Ilifuata fursa ya kuteua na kuunda serikali. Hapa napo alishindwa kabisa kuitumia. Aliwateua baadhi yao katika nafasi nyeti ndani ya chama na serikali. Wengine wakawa washauri wake wa karibu katika masuala nyeti ya kiserikali na kichama.


  Kwa kufanya hivyo, Kikwete alikosa fursa adimu ya kuwasikiliza wanachama na viongozi waadilifu wachache waliobakia katika chama.


  Kulikuwa na ripoti nyeti za kiusalama na za kamati za maadili. Rais alizipuuza na kuziita majungu na fitna; kisha akaendelea mbele kuwananga waliokuwa wanapigia kelele ufisadi. Ni wakati huo, Chama cha Jamii (CCJ) kilijitokeza kwa mara ya kwanza na kuwa gumzo na tishio kubwa kwa chama chake.


  Kuna taarifa kuwa Kikwete alijulishwa kila hatua ya harakati za CCJ. Kwamba alipelekewa nyaraka za CCJ na ushahidi wa kuhusika kwa wana-CCM katika kuanzisha chama hicho. Inaelezwa alishauriwa azuie CCJ kusajiliwa ili kunusuru chama chake kugawanyika.


  Kwa mwana-CCM, tena kiongozi, kukiunga mkono chama kingine kwa kificho ni usaliti. Hata katika demokrasia zilizokomaa, ni ruksa kupingana na msimamo wa chama chako waziwazi, lakini si kujiunga na chama kingine kabla ya kwanza kujiondoa katika chama chako.


  Nimeshtushwa na matamshi ya Samwel Sitta kuwa ni jambo la kawaida kuwa na mazungumzo na vyama vingine katika masuala ya siasa. Kama ni suala la mazungumzo hilo si tatizo, lakini kilichoendelea wakati ule si mazungumzo, bali ni kuanzisha chama na waliokianzisha chama si wanachama wa kawaida, bali viongozi waandamizi ndani ya CCM. Usaliti wa namna hii, siku moja utazaa uhaini.


  Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kuwashupalia baadhi ya wana-CCM waliounga mkono hoja ya kuunda Tanganyika pale walipochukua fomu kugombea urais mwaka 1995. Alisema mwaka 1995 walikuwa wanatafuta rais wa Tanzania na siyo Tanganyika na kwamba wanaotaka urais wa Tanganyika wasubiri.


  Ni kwa msingi uleule, hii sasa ni fursa kwa Kikwete kuwaambia waanzilishi wa CCJ walio ndani ya CCM, kuwa waondoke wakaunde CCJ ili iwe rahisi kwao kutekeleza madhumuni yao. Hata kama chama si mama, lakini pia chama si koti la kuvaa na kuvua kila unapohisi kero ya joto au baridi.


  Kwa kuwa sasa ni dhahiri CCJ ilianzishwa na wana-CCM waliokerwa na sera za CCM, pamoja na kiongozi wake, yaani Rais Kikwete, sisi tulio wana-CCM msimamo, tuna mashaka na viongozi wa namna hii.

  Hii ni fursa adimu kwa Kikwete kuondokana nao bila kusikia uchungu wowote kwa sababu waliyataka wenyewe. Hata kama msimamo wao dhidi ya ufisadi ndani ya chama ni mzuri, lakini hili la kuunda chama kingine linawaondolea sifa ya kuendelea kuwa viongozi kwa sasa ndani ya chama chetu.


  Mwingine aweza kusema mbona akina Wassira waliokuwa wapinzani sasa ni mawaziri? Jibu ni rahisi kuwa, walikuwa wapinzani waziwazi, kisha wakarudi CCM mchana kweupe. Hawa wa CCJ ndani ya CCM walifanya kwa uficho na hatujui ni siri ngapi ziliondoka wakati huo na muda, fedha za chama na serikali vilitumika kuendesha shughuli za CCJ.

  Kwa kuwa Rais Kikwete huwa anapata kigugumizi kufanya maamuzi magumu kwa hofu ya kuumiza upande mmoja, hii ni fursa nzuri kwake kuwaudhi wote kwa haki na bila upendeleo wowote. Hii ina maana kuwa kazi ya kujivua gamba iendelee mbele bila hofu ya kuwa inaongozwa na wana-CCJ walio ndani ya CCM.


  Hali kadhalika wana-CCJ walio ndani ya CCM waondolewe kwa kosa la usaliti na hii ifanyike bila hofu ya kuwa Kikwete anashinikizwa na mafisadi kwa sababu hao mafisadi hawakuwatuma wakaunde chama ndani ya chama.


  Kikwete akiondokana na makundi haya mawili ndani ya CCM, atajijengea heshima na msimamo thabiti. Zaidi ya yote, atakiponyesha chama na hatari ya makundi yasiyokwisha na yanayoendelea kukidhoofisha chama chetu.
   
 2. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu umechelewa, unauza chai tu hapa! Kwani unaizungumzia ccj ipi? Hakuna iko chama kwa msajili wala wanachama wa chama hicho, kwani mwenyekiti wake ni nani? Na ofisi yake iko wapi? Tunawahitaji zaidi kwenye ccm hao unaowasema watolewe. Kama vipi toka wewe!
   
 3. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2011
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hii sasa ni fursa kwa Kikwete kuwaambia waanzilishi wa CCJ walio ndani ya CCM, kuwa waondoke wakaunde CCJ ili iwe rahisi kwao kutekeleza madhumuni yao. Hata kama chama si mama, lakini pia chama si koti la kuvaa na kuvua kila unapohisi kero ya joto au baridi.
  Kwa kuwa sasa ni dhahiri CCJ ilianzishwa na Samwel Sita, Bernard Membe, Dr Mwakyembe ,na Mwambalasa waliokerwa na sera za CCM, pamoja na kiongozi wake, yaani Rais Kikwete, sisi tulio wana-CCM msimamo, tuna mashaka na viongozi wa namna hii.
   
 4. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hahahaha James Milya na Parokwa mbona mnahangaika sana hivi Lowassa amewaaahidi nini hadi mnapoteze utu wenu na heshima ya kibinadamu kumtetea! Pelekeni huko ujinga wenu na CCJ yenu! James Millya muuliza vizuri Lowassa hivi ni lazima awe Rais wa Tanzania? Hakuna watanzania wengine wanaoweza kuwa Marais? Mbona ana watumia vibaya?
   
 5. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2011
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mpende msipende is still valid and hold water ,any other naration and Blaa!! Blaaaa!! is your effort ya kuwapakata wasaliti Samwel Sita, Mwakyembe,Membe na Nape,Hawa wasaliti ni lazima washughulikiwe na Vikao vijavyo vya chama, Sita and his Clique must go! go! go!
   
 6. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kwa watu wenye akili, hao unaowataja ndio afadhari wanaweza kupanda jukwaani na kuitetea ccm wakasikilizwa, sio huyo EL wako. Kazi uliyopewa ni ngumu sana ya kuwatetea hao watu. Kuwa mkweli, wafuate uwaambie ukweli kuwa kazi hiyo ni ngumu sana, kwa umri wako imekuzidi.
   
 7. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2011
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  My friend Edward hajatangaza kugombea U-Rais ,for your information sio dhambi kwa Lowasa kugombea U-Rais ni haki yake kikatiba Sisi wanachama wa CCM tunamhitaji hajawahi kukisaliti chama ,Ni Mwanachama mwaminifu wa CCM ,Utiihifu wake kwa chama hauna mashaka hata kidogo

  Wasaliti ni Samwel Sita(Urambo), Bernards Membe (Mtama) ,Nape Nauye
   
 8. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kweli akili ni nywele! Yani Lowassa anavyo nukaa na harufu mbaya ya Uchafu wa Ufisadi wewe Millya una mtetea! Atakua Rais wa Wamasai tena wamasai wajinga lakini sio wa Watanzania! Lowassa ananuka harufu mbaya sana! He will never ever been trusted by the people of Tanzania!
   
 9. J

  John Marwa JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WanaCCM wenzako ni hawa hapa James Millya,Fred Lowassa,Edward Lowassa,Rostam Aziz,Chenge,Parokwa ambea mmemnunua hivi karibuni! Acheni kabisa ujinga wenu wa kumsafisha Lowassa! Kama mnataka watanzania wamwamini Lowassa basi aonge live Tv zimuoneshe anavyo inama! Pamoja na hayo bado watanzania hawatamuamini!
   
 10. melxkb

  melxkb JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Aaaaaah!! ......ni nywele kweli! Andika tu kiswahili mkuu. Lakini umejitambulisha vizuri ndio maana EL mbaya kwako lakini walewale wenye kuwa tayari kukuuza kama samaki hali unakula nao meza moja hao eti kwako ni vinara, duu! ama kweli ukistaajabu ya Musa.........!!
   
 11. T

  Twasila JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,913
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  Niliwahi kuandika humu kuwa nani ndani ya ccm anayeweza kumpiga jiwe mwanamke aliyefumaniwa akizini au anayeweza kumfuata mwanaume
  Aliyezini na huyo mwanamke!?
   
 12. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #12
  Jun 2, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hawa ndugu wamepewa uwaziri watulie maana, wenyewe walijichanganya mahesabu. Wangeweza kabisa kuibukia CDM. Naona kama umaarufu wao kisiasa sasa ndio unaondoka. Lakini wanaweza kucheza kama Bacelona.:pound:
   
Loading...