Kwa mujibu wa sheria kuu na sheria ndogondogo za nchi hii hakuna anayeruhusiwa kupanda gari la abiria(usafiri wa umma) bila malipo.
Hata askari na maofisa wa majeshi mbalimbali hawaruhusiwi.
Kama mwanafunzi asiyepokea mshahara analipa angalau nusu ya nauli, je, askari aliyeajiriwa?
Tena wanafunzi wengine wazazi au walezi wao ni duni mno.
Hii ilianzia utawala wa Mwinyi, kuna kipindi wanafunzi wa Dar es salaam walipewa ofa ya kupanda bure ndipo wanajeshi nao wakasema nasisi tunalinda nchi twapanda bure. Na majeshi mengine yakafuata mkumbo.
Mimi naomba wanafunzi wapande bure hasa wa S/msingi.