[h=5]Familia moja ilishangazwa pale
walipopokea jeneza la marehemu
mama yao
aliyefariki nchini Marekani. Lilitumwa
na mmoja ya watoto wake wa kike.
Mwili ndani ya jeneza ulikuwa
umesongwa sana ndani ya jeneza
kiasi
kwamba uso wa marehemu ulikuwa
umegusa kioo cha jeneza!
Walipofungua jeneza, walikuta barua
juu ya merehemu, iliyosomeka
namna
hii:
"Wapendwa ndugu zangu,
nimeutuma mwili wa mama yetu
kwa ajili ya
mazishi, kwani imekuwa siku zote
hamu yake kubwa kuzikwa
nyumbani Machame, katika nyumba
ya ukoo. Samahani sikuweza kuja na
mwili kwani
nimenyimwa likizo kwani kuna
upungufu wa wafanyakazi hapa
kazini mwezi
huu.
Ndani ya jeneza, chini ya mwili wa
mama, kuna makopo 12 ya samaki
wa
makopo, paketi 10 za supu ya Royco
na chupa 8 za jam ya maembe.
Mgawane
hivi kwa jinsi mtakavyoamua nyinyi.
Katika miguu ya mama kuna pea
moja ya viatu vya Reebok namba 9
kwa ajili
ya mtoto mkubwa wa Mushi. Pia,
kuna pea mbili za viatu kwa ajili ya
watoto wa Urassa na Kwayu,
natumaini nitakuwa sijakosea
namba za miguu.
Nimemvalisha pia mama American
T-shirts 6, kubwa kabisa ni kwa ajili
ya
Manka, na zinazobaki ni za watoto
wake. Hizo jeans mpya 2 ambazo
mama
amezivaa ni za wavulana. Hiyo Swiss
watch mkono wake wa kushoto ni
zawadi ya Koku kwa ajili ya sikukuu
yake ya kutimiza miaka 21. Anti
Rebeka, hizo heleni, mkufu na pete
ambazo mama amevaa ni zako.
Hizo soksi 6 ambazo mama amevaa
wagaiwe wajomba. Tafadhali
mgawane kama
nilivyosema na kama kuna kitu
kingine mnahitaji, basi mnieleze
kwani
hali ya baba nayo siku hizi si nzuri
sana.
Dada yenu mpenzi,
Mama Manka[/h]