Maistro 1
JF-Expert Member
- Sep 4, 2015
- 422
- 181
Walimu wa wilaya ya Misungwi tumepeta laana ya kumkataa na kutompigia kura Mhe. Edward Ngoyai Lowassa kuwa Rais wetu. Walimu tunashurutishwa kuchangia madawati kwa lazima watendaji wa vijiji na kata wanatufuata majumbani mwetu au barabani wakidai ni agizo la Rais, ukikutwa huna hela au ukigoma kuchanga unapelekwa kituo cha polisi na kuwekwa ndani, na akitokea ukafikishwa mahakamani kesi inageuzwa na ina kuwa ya kuhamasisha wanakijiji wasichange yaani ni shida.
Hii siyo haki kwa mwalimu kumlazimisha na kumshurutisha kuchanga madawati, ingekuwa HIYARI hapo tusingekuwa na tatizo, watendaji wanadai eti ni sheria, kwahiyo ukikataa unafungwa, yawezekana kweli hii ni sheria labda sisi hatuijui, Please tunaomba wanasheria mtuwekee hiyo sheria hapa labda inaweza ikatupunguzia hasira.
Walimu tunakatwa kodi ya mapato kwenye mishahara yetu kila mwezi na baadhi yetu inafika hadi Tshs.145000 so kwa mwaka ni Tsh.1,740,000. Swali la msingi ni hii kodi huwa ya nini? Na kama wanataka tuchange kama wanajamii wengine basi watupunguziwe kodi angalau ifike 30,000 maana na sisi kodi zingine za maisha ya mitaani tunalipa.
Baadhi ya walimu bado mpaka sasa tunaidai serikali malimbikizo au mapujo ya mishahara yetu na tunaona iko kimya. Mbona sisi hatujaipeleka mahakani na kuishitaki? Na mbaya kabisa baadhi ya walimu tulisimamia mitihani ya kidato cha IV mwaka jana novemba mpaka leo hii hatujilipwa baadhi ya posho zetu, so tunaidai serikali, mbona hatujaipeleka mahakamani?
Shule nyingi na karibia zote za Misungwi ni za kata so hazina laboratory technicians so walimu wa masomo ndiyo laboratory technicians na ikumbukwe kwamba ma - technician ni watalaamu kama walivyo wengine so wanatakiwa kuajiliwa na serikali. Ila hawapo na taluma hii inaonekana kama vile haipo au imekufa, So walimu wa masomo tunafanya kazi ya walimu wawili bila posho yoyote wala kifuta jacho, mbona sisi hatujaipeleka serikali mahakamani? maana tunafanya kazi ya mtu mwingine kabisa anayetakiwa kulipwa mshahara na serikali ila sisi tunaifanya bure na kwa kujitolea na bila posho yoyote.
Je hii nini? Bila shaka na kupepesa macho hii ni laana ya kumkakataa Lowassa na baadhi ya walimu tuliipigia chapuo CCM na kuinadi kwa kila namna sasa tunaisoma namba aka tunajuta na kumkumbuka Lowassa, 'Kweli CCM Ni Ile Ile' na baadhi yetu tunaona angalau wakati wa Kikwete tulikuwa tunaheshimika, pamoja kuwa kulikuwa na michango wakati wa Kikwete ila tuliichanga kwa HIYARI siyo ya sasa hii ya kudhalilishwa na kuwekana lupango. Hii inatakiwa iwekwe kwenye maajabu ya kumi ya ulimwengu 'yaani mwalimu una unafundishwa zaidi ya wanafunzi 600 wa sekondari kwa wiki kwa mshahara tu, na unalazimishwa kuwanunulia wanafuzi hao hao madawati '
KWELI TUMEPATA LAANA YA KUMKATAA LOWASSA