Walimu wenzangu: Hivi ukiwa mwalimu ni lazima uvae manguo yasiyoeleweka, oversize na malonya?

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
69,804
137,090
Habari za jioni Jf........

Asilimia kubwa sana ya walimu nguo tunazovaa kwakweli kuna muda ukikaa kumtizama mtu unacheka kimoyo moyo, mwalimu wa kike unakuta kavaa gauni panaaa linaishia katikati ya miguu sio fupi sio refu, kama ni sketi basi sehemu ya hips imezidi inakua kama nguo ya kuazima, chini sandals, koti oversize, wengine hadi na nywele twende kilioni......vivyo hivo walimu wa kiume shati bongee la shati mkono unashindwa kujua ni la mikono mifupi au mirefu, suruali buga (bwanga) mkanda haujulikani rangi, mkanda mrefu unazungushwa kama kanga... Hii ni kwa ufupi ila tuna mengi mno.

Walimu kwanini tunavaa hivi? Tumeshindwa kutofautisha kati ya haiba na kuwa smart?? Haiba ni kuvaa nguo oversize au lonya? Au ni akili tu tumezitune manguo ya ajabu ajabu ndo yetu? Sijui wanafunzi huwa wanawatuwazia nini...

Cha ajabu hata walimu wanafunzi nao wanakuja field nguo wanazovaa mmh, naishia kuwaza nnavowajua Wanachuo vivazi vyao wakiwa chuo, very smart wanakuja field utadhani ni watu wametoka vijijini, sketi imeungwa vipande saba yani ipo kama kabeji
Tujirekebishe jamani haiba sio kuvaa malonya
 
IMG-20170209-WA0115.jpg
IMG-20170209-WA0128.jpg
.
Gauni za heshima na unaonekana smart, ila tunavopenda malonya sasa :D:D
 
Kama wewe ni mwalimu kuna kitu kinaitwa haiba..... Hutakiwi kuvaa maronya kama unavosema vaa nguo inayokukaa ila yenye haiba
Sio unavaa kigauni kama icho ulichotuma then unaingia drs la sita, saba au secondary unategemea mwanfnz akuelewe.

Utaandika ubaoni uku nyuma wanafunz wanajadili mapaja na magoti ya mwalim.
 
Kiongozi miye nadhani watangulizi ndio role model wao kimavazi wewe angalia tu kila kada dressing zao zina fanana angalia
Askari kutwa na jezi au traki suti
Mwalimu ndio hivyo sasa wana mashati yao sasa ya mandela, suruali za kadeti za kariakoo yani haaaa haaa
 
Nguo kama hii haistail mwalim kuingia nayo drsan.... Ukinyoosha mkono kuandika tarehe ubaon nusu ya paja nje, ukidondosha chaki huokoti......

Noo mavaz ya ualimu yana haiba but sio midabwada
Unajiongeza inavuka goti, iwe fupi ya kawaida sio katikati ya miguu sio fupi sio ndefu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom