Hii sheria nakumbuka wakati inapitishwa ilileta kelele sana na moja sehemu iliyopigiwa kelele ni hilo unalolisema wewe,yaani inatosha kabisa kwenda jela kwa kutajwa na binti kwamba katembea na wewe hata kama tendo lilifanyika siku za nyuma yaani pasipo ushahidi wa kidakitari.Hivi binti kumtaja mtu ni ushahidi tosha wa kumtia mtu hatiani? Na je kama hii kesi ilisukwa ili binti amataje mtu ambaye hausiki? Kwa hukumu kama hii sio suala la kushangilia, kwa muktadha huu kila mtu hayupo salama hata wewe hapo unaweza kuundiwa ili zengwe na hata kama ni wew ni mwanamke ndugu yako au mme wako au mtoto wako anaweza kupatwa hili suala.
Kumfinyia jicho msichana/mwanamke,kushika makalio yake au matiti pasipo idhini yake pia ni kubaka hivyo kazi kwenu..,kama wanawake wengi wangetaka kuitumia hii sheria magereza yangefurika wabakaji.