Walimu wasibaniwe kwanda kusoma kozi za ict.

Walimu wasibaniwe kwanda kusoma kozi za ict.

TANZANIAN NINJA

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2018
Posts
455
Reaction score
541
Amani iwe nanyi wanajamvi! Kwa mawazo yangu kwakweli walimu wangeruhusiwa kwenda kusoma masomo ya ICT au I.T na kupewa likizo ya malipo hata ikiwezekana alipiwe kabisa na ada tofauti na ilivyo sasa mwalimu akitaka kusomea masomo ya ict basi inampasa kuomba rikizo bila malipo kwa madai ya kwamba ati anasoma fan tofauti na ualimu.
Nikweli kwamba mwalimu akitaka kusoma fani tofauti na ualimu ni lazima aombe rikizo bila malipo lakini kwa mtazamo wangu kwa hizi kozi zinazohusiana na computer wangepewa tu fursa ya kusoma kama vile ambavyo angesoma fani ya elimu kwa sababu kwa kiasi kikubwa fani za kompyuta zinahusiana na kazi ya ualimu hasa ukizingatia kunamasomo ya ICT na TEHAMA.
Angalau basi kozi ya ict with education au education with ict serikali ingetilia mkazo ili walimu wajiunge huko, UDOM waliwahi kuwa na hizo kozi za elimu na ict sijui ziliishia wapi maana zimepotea tu hewani.
Masomo ambayo ni muhimu kwa dunia ya sasa cha ajabu katika shule zetu za ktz ndio yanachukuliwa poa mfano stadi za kazi, na ict/tehama.
Huu ni mtazamo tu.
 
Nimesoma iyo kozi udom kaka ila mpaka sasa hakuna ajira wala nini ila kwa sasa niko na project ya kuanzisha mafunzo ya basic of ict kwa tanga mjini hii itakuwa mahususi kwa waalim,ivyo nahitaji mtaalam wa it anayeweza pia kuwa na market stategy nzuri ajee pm tuyajenge this is for only serious person
 
Mwandiko wa Mwl huu! No paragraphs! Anaandika tu!
 
Nimesoma iyo kozi udom kaka ila mpaka sasa hakuna ajira wala nini ila kwa sasa niko na project ya kuanzisha mafunzo ya basic of ict kwa tanga mjini hii itakuwa mahususi kwa waalim,ivyo nahitaji mtaalam wa it anayeweza pia kuwa na market stategy nzuri ajee pm tuyajenge this is for only serious person
Nimeku pm ndugu..
 
Hadi na wewe umeacha paragraph...!

Kosa:umeandika Mwl badala ya Mwl.

Ulivyokuwa pimbi unakimbilia kukosoa kweli nyani haoni kundule

Mi sio Mwalimu, siwezi kumuita binadamu mwenzangu Pimbi!
 
sasa mkuu huo mwongozo uko sahihi sijaona kama wamenyanyaswa Ualimu ni Taaluma tofauti na ICT AU IT isipokuwa unaweza kusoma Education with ICT au IT hujabaniwa isipokuwa kusoma hiyo kozi ya elimu na ict lazima uwe umesoma masomo ya sayansi.

Ukisema hivo na kada zote zitadai kwenda kusomea vitu vingine, Kesho Nes naye atadai akasome ICT, au IT so sijaona ubaya.
 
Sawa mkuu ingekuwa vema na kozi ya ict na elimu wangeipa mkazo
 
Sawa mkuu ingekuwa vema na kozi ya ict na elimu wangeipa mkazo
mkuu mkazo upo tena isipokuwa hujafanya uchunguzi
1.ualimu ngazi ya cheti kuna somo la ict na nahis nowdays wanalifanyia mtihani.

2.ualimu dplm pia vyuo vingi vina somo la ICT tena kwa vitendo

3.Vyuo vikuu cna uhakika kama kila kozi ya elimu wanasoma ICT so mkazo upo ila shida ni vifaa maana chuoni wanasoma hilo soma isipokuwa COMPUTA zipo ngap na wanaosoma ni wangap??

So mkazo upo mkuu.
 
Nimesoma iyo kozi udom kaka ila mpaka sasa hakuna ajira wala nini ila kwa sasa niko na project ya kuanzisha mafunzo ya basic of ict kwa tanga mjini hii itakuwa mahususi kwa waalim,ivyo nahitaji mtaalam wa it anayeweza pia kuwa na market stategy nzuri ajee pm tuyajenge this is for only serious person
Nipo Tanga mjini nina dip ya uandishi siwezi kufit hapo tukasaidiana kaka
 
Back
Top Bottom