Walimu wapya waahidiwa kuishi Kifalme mkoani Kigoma

Walimu wapya waahidiwa kuishi Kifalme mkoani Kigoma

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,065
Reaction score
64,218
Walimu wapya waahidiwa kuishi Kifalme mkoani Kigoma....Watapokelewa katika vituo vya mabasi na Reli kwa mabango.....Wavuvi kila siku kuwaletea Samaki nyumbani kwao

KATIKA utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), Halmashauri ya Wilaya Kigoma, imeamua kuwapokea walimu wapya 430, kwa mbinu ya pekee ili wabaki katika vituo vyao vya kazi. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kigoma, Miriam Mbaga, alitangaza mbinu hizo jana wakati
alipozungumza kwenye kikao cha maandalizi ya mapokezihayo.

Alisema pamoja na maandalizi mengine, halmashauri hiyo imetenga Sh milioni 25 kwa ajili ya kuwapa walimu hao fedha za kujikimu wakati wakishughulikia maandalizi ya kwenda kwenyevituo vyao vya kazi.

Fedha hizo ni nje ya kiwango cha fedha kilichotengwa na Serikali kwa ajili ya kujikimu, ambacho kila mwalimu atakayeripoti atapewa kimsaidie kujikimu kwa siku saba.

Sambamba na posho hiyo, Mkurugenzi huyo alisema kuwa pia katika kuhakikisha wanawapokea walimu wao kifalme,halmashauri itampatia kila mwalimu godoro moja na taa yakuchaji, ambavyo vinatolewa kama motisha kwa walimu hao wapya.

Mbaga alisema kuwa wakati motisha hiyo ikitolewa, pia timu ya watumishi wa halmashauri imejipanga kuwapokea walimu watakaoripoti katika vituo vya mabasi na kituo kikuu cha reli mjini Kigoma.

Wakati wa mapokezi hayo, watumishi hao watakwenda katika vituo husika wakiwa na mabango yanayoashiria mapokezi ya walimu na baada ya kuwapokea, watawapeleka katika nyumba za kulala wageni watakapoishi wakisubiri utaratibu wa kiutumishi wa kuwapatia makazi.

Mkurugenzi huyo wa halmashauri amebainisha kwamba wakati katika ngazi ya halmashauri maandalizi yakiendelea hivyo,katika ngazi za vijiji, viongozi wa vijiji wamekutana na kuanza maandalizi ya kuwatafutia walimu wapya nyumba za kuishi zenye hadhi ya kuishi walimu hao kwa ngazi ya kijiji.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kigalye, kilichopo Kaskazini ya Mwambao wa Ziwa Tanganyika, Hussein Mussa Kasala,alisema tayari Halmashauri ya Kijiji hicho imekutana na kutafuta nyumba nne.

Nyumba hizo kwa mujibu wa Kasala, zinakidhi mahitaji ya familia nane za walimu hao; zimejengwa kwa matofali na zipo katika mazingira mazuri ya kuishi walimu.

Mwenyekiti huyo wa Kijiji alisema kuwa wanakijiji wamejipanga kuwapokea walimu hao kwa kuwapatia magunia ya mahindi na maharage, kwa ajili ya kuanzia maisha huku wavuvi wakiahidi kuwapatia samaki na dagaa kila watakapokuwa wakirudi kutoka ziwani.

Akielezea hali hiyo, Mbaga alisema kuwa utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa, unaanzia kwa mtu mmoja mmoja kama ambavyo halmashauri za vijiji zimeamua kuchukua hatua kutekeleza jambo hilo kulingana na rasilimali zinazowazunguka.

Naye Meneja wa benki ya CRDB, tawi la Kigoma, Philemon Pindapinda, ambaye alikuwa mmoja wa viongozi wa sekta binafsi na sekta ya umma walioalikwa kuhudhuria maandalizi ya mapokezi hayo, alisema hatua iliyofikiwa itawatia moyo walimu kuona namna ambavyo utumishi wao unakuwa na maana kwa jamii.

Pindapinda alisema nia ni kuona walimu wanaopangiwa mkoani humo hasa katika maeneo yanayoonekana kuwa na miundo mbinu duni ya usafiri, wanaripoti na kukubali kuishi katika mazingira hayo na kufanya kazi yao kwa moyo.

Mhasibu Mkuu wa Benki ya Posta (TPB) tawi la Kigoma, Ahmed Soso, alisema maandalizi yanayofanywa na Halmashauri ya Wilaya Kigoma, yanapaswa kuwa mfano wa kuigwa na halmashauri nyingine za mkoa huo, ili kuwaonesha moyo wa upendo watumishi hao wa sekta ya elimu ili waripoti na kukaa kwenye vituo walivyopangiwa badala ya kukimbia.

Source: Mpekuzi
 
Ni mbinu nzuri ya kuwashawishi walimu kuripoti kigoma, ila wasiwasi wangu isije ikawa ni mbinu ya mkurugenzi na wasaidizi wake kupiga hela ya umma kupitia hizo offer wanazozitoa kwa walimu! Tazama kuna posho za kikao maalum cha kamati za mapokezi, hela za mabango, per diem kwa watakaoshinda stendi na station kusuburi ugeni, gharama za gesti kwa wageni, chakula cha wageni n.k n.k! Nachelea kusema hapa pana password inatafutwa!
 
geografia ya wilaya ya kigoma ni ngumu sana. kuna baadhi ya tarafa ni ngumu sana. kwa mfano maeneo ya Tarafa ya Kalya na Buhingu iliyoko mwambao wa kusini wa ziwa Tanganyika hakuna barabara, usafiri ni meli na boti. meli inatembea mara mbili kwa mwezi, nauli ni elfu ishirini na tano (kwenda na kurudi ni elfu hamsini). hizo boti ni za mbao zinapakia sana na hali ya ziwa mara nyingi si shwari. kutoka kigoma mjini hadi tarafa za kalya na buhingu ni safari ya zaidi ya saa 10 na mara nyingi safari hufanyika usiku

mawasiliano ya simu hakuna, kutoka kalya hadi kwenye kichuguu ambapo network inapatikana, nauli ni shilingi elfu kumi kwa pikipiki.
kitu pekee utakachokifurahia ni uhuru, maafisa na waajiri hawafiki kabisa maeneo hayo kutokana na ugumu wake

siwatishii ila huo ndio ukweli wa mambo
 
hapana. huyu mkurugenzi yuko vizuri sana hakika nakuambia


Ni mbinu nzuri ya kuwashawishi walimu kuripoti kigoma, ila wasiwasi wangu isije ikawa ni mbinu ya mkurugenzi na wasaidizi wake kupiga hela ya umma kupitia hizo offer wanazozitoa kwa walimu! Tazama kuna posho za kikao maalum cha kamati za mapokezi, hela za mabango, per diem kwa watakaoshinda stendi na station kusuburi ugeni, gharama za gesti kwa wageni, chakula cha wageni n.k n.k! Nachelea kusema hapa pana password inatafutwa!
 
Posho mil 25 kwa walimu 430,Godoro na taa ya kuchaji ndiyo kuishi kifalme!ukistaajabu ya Musa utayaona ya Kigoma.
 
Hongera kwa hiyo motisha, lakini angewaonjesha posho ya jamaa waliopo dodoma hao walimu walau kwa wiki moja.
 
mil25 kwa walimu 430 ni elf 58 kila mmoja na taa ya kuchaji ya buku jelo dah maisha ya kifalme hayo
 
Mkuu TISA DISEMBA, nakubaliana na wewe mia kwa mia katika mawazo yako, wabongo ni wapga dili sana, hapo watu wanashangilia motisha, huku nyuma watu wanapga mpunga. Halafu eti kila siku watapata mgao wa samaki bure, thubutu, nimeishi huko kigoma, mha ni mbishi balaa.
 
Mkuu TISA DISEMBA, nakubaliana na wewe mia kwa mia katika mawazo yako, wabongo ni wapga dili sana, hapo watu wanashangilia motisha, huku nyuma watu wanapga mpunga. Halafu eti kila siku watapata mgao wa samaki bure, thubutu, nimeishi huko kigoma, mha ni mbishi balaa.

Natusubiri tuone! Kigoma wakiweza, wengine waige!
 
Hakuna na haitatokea kitu kama hicho, ila jamani walimu twenden tukawasaidie ndugu zetu wa kigoma wakati tunawasubiria vijana wale walioenda kujifunza uzalendo juz jeshini wamalize masomo wapangiwe huko mnakopaogopa eti kwa madai mazingira magumu,hao vijana a.k.a majeda wataenda okoa jahaz au vijana mliotoka jeshin juz hamtaenda kigoma?
 
Huyu mama jamani anaweza hata mwaka jana aliweza kuwapa usafiri walimu waliopangiwa vijiji vya mbali na yeye mwenyewe aliwasindikiza ila kwa bahati mbaya anahama Kigoma.
 
Back
Top Bottom