Walimu wapya msisahau kutumia P Two na Con

Mwl wa akiba

Member
Nov 12, 2020
66
66
KWENU WALIMU WAPYA: MSISAHAU KUTUMIA P TWO NA CON...🤔

Naandika Mwl wa akiba

📌Itoshe kusema kuwa wale wote ambao mmebahatika kupata ajira mpya za ualimu tambueni kwamba mmeaminiwa na nyie muaminike sasa mkachape kazi kwa bidii.

📌Napenda kuwakumbusha kwamba msisahau kutumia kwa ubobezi na uweledi wa hali ya juu zile P mbili . NA CO Moja , ili mchakato wa ujifunzaji na ufundishaji uende kiuweledi naomba niwakumbushe kama ifuatavyo

CONTENT KNOWLEDGE 📌
Kwa lugha rahisi huu ni ule ujumbe /mada/ maudhui yanayowasilishwa hivyo Mwalimu unatakiwa utambue Content Yako kwa hali ya juu sana na kwa mawanda mapana ili wanafunzi wafaidike na wewe na ili kujiboresha lazima usiwe mzito kujisomea katika vyanzo mbalimbali vitabu na mitandao na kwa walimu wengine pia hii itakujenga sana kama Mwalimu.

PEDAGOGY KNOWLEDGE
📌(P 1)
Hii ni P ya Kwanza kwa maana rahisi ni inahusika na namna ya uwasilishaji wa maaudhi kwa wanafunzi hapa mwalimu lazima awe anafahamu namna ya kuwasilisha kwa wanafunzi uku akizingatia utofauti wa kiuwezo wa wanafunzi lakini pia mbinu changamfu na jumuishi katika uwasilishaji wake .

📌Lakini katika Pedagogy knowledge lazima mwalimu asisahau kuhusianisha kile ambacho anakiwasilisha na mazingira ya eneo husika au taifa hivyo mwalimu hapa inabidi ajikite kwenye kutambua wanafunzi wake kiundani kabisa .

PROFESSION KNOWLEDGE ( P )📌

Baada ya mwalimu kuwa mbobezi kwa anachokiwasilisha na namna ya kuwasilisha ni lazima mwasilishaji naye awe mbobezi kuhusu taaluma yake kiundani zaidi maana hapo ndio msingi ulipo zaidi.

📌Hivyo Mwalimu lazima atambue haki na wajibu wake na atimize kikamilifu kabisa na ajue kabisa ana wajibu gani kwa mwanafunzi ,taaluma, mwajiri ,jamii na azitambue haki zake na azitetee kwa uweledi na umakini bila kusahau kutimiza wajibu .

📌Endapo walimu wapya wakitumia kwa ubobezi na uweledi wa hali ya juu maarifa hayo matatu kwa mwalimu kuna hatua chanya tutapiga kama taifa na wataihesimisha taaluma ya ualimu .

P2+ C knowledge= PCK


NB : WALIMU WA KIUME KABLA YA KUMPA SHETANI NAFASI BASI MIAKA YAKO ONGEZA MIAKA 30 KISHA TAFAKARI 😂😂😂

Wenu katika kusubiri

Mwl, wa Akiba
 
Back
Top Bottom