Walimu wapata Chama mbadala cha kuwatetea

Walimu wapata Chama mbadala cha kuwatetea

Mei mosi kilipigwa mkwara
Nani aliyekipiga mkwara, na kwa nini? Maana mfanyakazi ana haki ya kujiunga na chama chochote kile cha wafanyakazi akipendacho.

Na kwa bahati mbaya CWT wamekithiri kwa wizi na ubadhirifu wa kutisha wa pesa za walimu! Wamekuwa wakiwakata walimu ada ya uanachama kwa mfumo kandamizi na wa kinyonyaji, wa asilimia! Badala ya ule wa makato sawa kwa wananchama wote!

All the best kwa chama kipya. Natamani kuona siku moja walimu wote wenye akili timamu wanatoka huko CWT, halafu tuone mwisho wa CCM na mtoto wake CWT.
 
Hata Azam tv wakati wanaanza kurusha matangazo yao, malipo yao kwa mwezi ilikua elfu 12 tu!!! Wenyewe wanakuambia AzamTv burudani kwa wote.....leo hii vipi? Burudani kwa wote inaendelea?
1. Chama kipya mwalimu ameomba kuingia mwenyewe, ameomba kukatwa 5,000 mwenyewe so mwajiri hawezi kubadili hicho kiasi kamwe .

Je ni mwalimu yupi aliandika barua kuomba kukatwa 2% ?
2. Wizi ni mkubwa CWT na wamefilisika hatua Hata hawataki kusikiliza sauti ya Mama Samia, wana Rais wao.
3. Rushwa CWT kwenye chaguo zao ni 100%
4. Kuanguka kwa elimu nchini kumechangiwa na CWT.
5. Saccos wemeziweka kutoa mikopo ya kunyonya damu walimu. Wanachukua fedha bank zenye riba, wanamkopesha mwalimu kwa riba.
Matokeo yake mwalimu analipa riba ya bank, riba ya saccos na wakati huo huo , walimu Anayo let’s say 5,000,000 huko saccos,anapewa mkopo wa 10,000,00 Kumbe imeongezewa hapo ile amana yake mwalimu analipa riba inayotokana na 10,000,000.
 
Bila shaka unamanisha walimu Wana mioyo kigumu ya kuwa wanachama wa CWT,ni kweli lakini jiulize nani anawapa nguvu CWT ya kuwaibia walimu bila uwoga wowote? Na je kama wanalindwa kiasi hicho wanaweza kuwakosoa wanao walinda?
Chartism+ Luddism



Namaanisha hao Viongozi wawakilishi wa chama inavyosemekana kutafuta michango ya walimu,
Yaani hata dhamiri zao naona zilishakufaga zamani!

Wenzeni mishahara yenyewe haitoshi halafu bado mnawapiga ?!
Halafu wanachokifanya ni kipi ?
Mishahara hupanda ipendavyo serikali.
Yaani kifupi bila hivyo vyama maisha yanaendelea salama tu.
Je maslahi gani ya watumishi wanayopigania na kupatikana?
Yanaweza kuhesabiwa na kuonekana?
 
walimu ni watu wa hovyo itoshe kusema tu hayo, Nawasilisha.
Kama unasema hili kwa nia njema fafanua ni kwa jinsi gani walimu ni watu wa hovyo.Vinginevyo tutaelewa umekariri tu kwa kusikia wengine wanasema hivyo,au wee ni mvuta bangi tu na hakuna kingine chenye maana maishani mwako isipokuwa bangi.
 
Huwaga mnpayuka Kwa kumlaumu mwalimu bila kujua Hali halisi !! Huwa namshangaa Sana mtu anaeponda walimu bila sababu za msingi!? Hivi unawezaje kusema mtu ni WA hovyo!? Wewe ni WA.maana kiasi Gani!?una Nini!?
Kuna wakati mtu analazimika kusema hivyo, binafsi nimewahi kuwa mwl..kada hiyo inaongoza kwa unafiki wa wao kwa wao, kusengenyana, wivu, kuchongeana kwa viongozi, kujipendekeza na vitabia vingi vya aina hiyo...
 
Kuna wakati mtu analazimika kusema hivyo, binafsi nimewahi kuwa mwl..kada hiyo inaongoza kwa unafiki wa wao kwa wao, kusengenyana, wivu, kuchongeana kwa viongozi, kujipendekeza na vitabia vingi vya aina hiyo...
Hakuna kada iliyo nyooka,hata ukienda jeshini vilio vya watu kuchongeana ni vingi sana,ni hulka za watu walio kwenye kada mbali mbali.
 
Back
Top Bottom