Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 8,273
- 25,303
Arusha . Serikali imewaonya walimu wanaojihusisha na mahusiano ya kingono na wanafunzi wao, kwamba watachukuliwa hatua kali za kisheria watakapobainika.
Katibu Mkuu wa Tume ya Utumishi wa Walimu Tanzania (TSC), Winifrida Gaspa Rutaindurwa ametoa onyo hilo leo Ijumaa alipokutana na wadau wa kielimu wakiwemo walimu wakuu, waratibu elimu na maofisa elimu na walimu katika semina ya maadili na nidhamu iliyofanyika Chuo cha ualimu Monduli mkoani Arusha.
"Walimu naomba tukemee vitendo vya mahusiano mashuleni na mimba za utotoni na tusiwe chanzo cha kujihusisha na ngono,"alisema
Rutaindurwa amesema kumekuwepo na wimbi kubwa la vitendo vya mapenzi ya jinsi moja kwa wanaume na mimba za utotoni matukio yanayosababishwa na ukosefu wa maadili na malezi.
“Niwaombe walimu wangu na wadau wote wa elimu muwaelimishe wazazi juu ya kufuatilia mienendo ya watoto wao hasa nyakati wakiwa likizo au wanaporudi nyumbani jioni, lakini pia wachunguzwe kwa ukaribu urafiki walionao na watoto wengine,”amesema
Kwa upande wake mkurugenzi msaidizi wa tume hiyo upande wa ajira na maendeleo ya walimu, Mectildis Kapinga amewataka walimu kutoa taarifa mapema pindi wanapochukuliwa hatua za kinidhamu na mamlaka zisizohusika kwani kuwafanyia hivyo ni ukiukwaji wa kanuni na sheria na taratibu za utumishi
“Ziko mamlaka nyingi siku za hivi karibuni zinawapa walimu adhabu mbalimbali za kumfukuza kazi au kumsimamisha kazi au kumpatia adhabu ya viboko na zingine, lakini niseme kuwa sheria namba 25 ya 2015 hairuhusu mamlaka nje ya tume ya utumishi wa walimu kumuadhibu mwalimu,"amesema.
Chanzo: Mwananchi