MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,252
- 8,003
Naomba walimu wanisamehe bure maana huu ndio ukweli wenyewe halisi wa hali ilivyo mtaani.
Zamani walimu Walizoea kukusanya pesa kutoka kwa wanafunzi kwa ajili ya masomo ya ziada yaani tuition. Sasa kufuatia agizo la serikali kwa agizo lake la Elimu bure na hakuna mwanafunzi atayechangishwa mchango wa aina yeyote imekua ni mwiba mkali sana kwa walimu hali inayowapelekea kuishi maisha magumu tofauti na awali.
Nimekutana na walimu watatu wakilia kwa sauti zinazofanana juu ya uamuzi huu wa serili na kuona ualimu ni kama kazi ya adhabu! Sasa wengine wanafikiria hata kutafuta madarasa nje ya shule na kuwatangazia wanafunzi hao hao wakutane nao huko huko.
" Kama darasa Lina wanafunzi 200 inamaana ukichangisha sh 1000 kilamwanafunzi kila mwezi inamaana utapata sh200,000 ambayo inakusaidia kwa mahitaji yako mengine,lakini sasa hatuna namna maisha yamekua magumu mno" hii ilikua ni kauli ya mwalimu moja wa shule moja ya sekondari hapa mkoani!
Kwa hali hii serikali iwafikirie wafanyakazi hawa zaidi maana kwa sasa hawana amani kabisa na maisha yao na wala hawafurahii kazi yao kama wafanyakazi wengine.