Walimu wamebebeshwa zigo la Elimu bure

kingunge wa jf

JF-Expert Member
Dec 24, 2013
455
424
Nianze kwa kutoa pole kwa watumishi wenzangu hususani walimu. Poleni sana.
Nimefafakari na kuona mateso mnayopitia kwa sasa katika utumishi nikaona wacha tusaidiane kupumua. Maana hali si hali.

Pamoja na hali ngumu hapo nyuma iliyokuwepo kabla ya serikali rais Magufuli kuingia madarakani kwa sasa mambo yamekuwa Magumu zaidi kwa walimu. Labda ule msemo uliozoeleka unaosema 'Mchawi wa teacher ni teacher'

Tangu kuasisiwa kwa elimu bure nchini chini ya utawala wa mwalimu mwenzetu, gharama na mzigo huu umewaendea watumishi hususani walimu kwa sababu tangu mpango wa 'elimu bure' uanze ulienda na madaraja ya walimu kitu ambacho kilikuwa ndio tegemeo kwa ustawi wa mwalimu. Kauli za mkulu za kusema hataongeza mshahara kwa sababu ana mambo mengi ya kufanya ni pamoja na hili ya kusomesha watoto bure.

Walimu walioajiriwa 2012 2013 na 2014 wote walitegemea kupata madaraja yao toka mwaka 2016 lkn mpaka sasa hawana vyeo hivyo ama promotion ya aina yeyote badala yake wameishia kupata 7000 baada ya miaka miwili bila increments.

Pamoja na kwamba serikali inajinasibu kufanya mambo mengi kwa gharama na maumivu ya wafanyakazi lkn hata serikali ya awamu iliyopita ilifanya haya huku watumishi hususani walimu wakiwa angalau wanastawi.

Ni jambo la kushangaza mwalimu kukaa miaka 6 bado akiwa anatumikia cheo kimoja kisa unatoa elimu bure. Kuna haja gani ya kutoa elimu bure wakati mwalimu ana hali mbaya?

Mwisho, ni wito wangu kwa vyama vya wafanyakazi hususani CWT. Pamoja na tishio kubwa la kunyimwa uhuru wa kujieleza nadhani mnayo nafasi ya kutafta forum mkapaza sauti juu ya walimu. Uoga ni dhambi.
 
Ngoja tuone anatupeleka wapi huenda anayo nia njema tu na watu wake.... Tumpe muda
 
Fedha za walimu zinatumika kuwalipa wasiojulikana, kulipia gharama za fiesta uwanja wa taifa, kununua madiwani na wabunge purura wa upinzani aka wachumia tumbo. Nk.
 
Back
Top Bottom