Walimu wakuu na wakuu wa shule za Serikali wapewe mamlaka yakufukuza walimu wasiowajibika ipasavyo

Vasco wa degamer

Senior Member
Feb 21, 2016
194
144
Ili kubadili na kupunguza kuporomoka kwa elimu yetu, maamuzi yanatakiwa yatolewe juu na walimu wakuu na wakuu wa shule za Serikali.

Ili mwalimu akifundisha ajisikiavyo/kizembe kizembe yeye afukuzwe tu bila kusubiri mwajiri wake/mkurugenzi, kama ilivyo kwa shule binafsi.
 
Ili kubadili na kupunguza kuporomoka kwa elimu yetu, maamzi yanatakiwa yatolewe juu na walimu wakuu na wakuu wa shule, ili mwalimu akifundisha ajisikiavyo/kizembe kizembe yeye afukuzwe tu bila kusubili mwajiri wake/mkurugenzi, kama ilivyo kwa shule binafsi.
Mwisho tutavunja Sheria (ultra vires). Mamlaka ya ajira ya waalimu ni Waalimu wakuu?
 
Kwani shule binafsi wao wanafanyeje kuwathibiti walimu wasiowajibika?
That's why nimesema:) wapewe mamlaka juu ya walimu wao,
mwalimu anafika shule saa mbili asubuhi, anaanza kujiulize afundishe siku hiyo au aache, akijisikia anaingia darasani anafundisha dak 20 anaondoka kesho inakuwa the same situation, wakati anajua anapaswa kufundisha vipindi vingapi daily.
 
Ili kubadili na kupunguza kuporomoka kwa elimu yetu, maamzi yanatakiwa yatolewe juu na walimu wakuu na wakuu wa shule, ili mwalimu akifundisha ajisikiavyo/kizembe kizembe yeye afukuzwe tu bila kusubili mwajiri wake/mkurugenzi, kama ilivyo kwa shule binafsi.
Tunapaswa kuzingatia utawala wa sheria la sivyo wengi watafukuzwa kwa sababu na chuki binafsi
 
Ili kubadili na kupunguza kuporomoka kwa elimu yetu, maamzi yanatakiwa yatolewe juu na walimu wakuu na wakuu wa shule, ili mwalimu akifundisha ajisikiavyo/kizembe kizembe yeye afukuzwe tu bila kusubili mwajiri wake/mkurugenzi, kama ilivyo kwa shule binafsi.
mbona mmewasakama walimu? Kwani ni idara pekee iliyo shindwa kuliko idara zote serikalini? Mbona kuna idara zimeshindwa kabisa zaid ya elimu?kuna ngazi husika zinazo shughulikia kufukuzwa kazi na na haziwezi kutolewa maamuzi na mtu mmoja kutakuwa na uvunjaji mkubwa sana wa haki za wafanyakazi, nadhan hukutumia akili yako kutafakari kabla huja post,tuwe na tabia ya kutafakari pande zote ili kuwa na jibu sahihu sio kuja na majibu ya upande mmoja.
 
Shida ni kwamba kuna wengine watatimuana kwa chuki binafsi..si unajua binadamu ni dhaifu.
 
umeongea pumba sana asee iv akiwa na kisa na mwalim si ndo atamtmua mda wowote? fikiria kwanza sio lazma ukiwaza ulev wako uulete hapa
 
Unamuongelea huyu mwalimu mkuu ambaye ana bifu na mtaaluma wake tangu mwaka jana kisa wote wanapiga yule demu wa mgahawani mzuri kuliko wote hapa kijijini?
 
Nilijua utasema shule zipewe mamlaka kamili ya kujiendesha mfano.kudahili upya wanafunzi tunaoletewa, michujo kwa kila darasa ili yule anayefeli abak darasa lile lile wenzake wakiendelea. Shule zipewe fedha kununua vitabu kulingana na mahitaji yake kwa sasa serikali ndo mnunuz mkuu.
 
Kuna mambo mengine hayawezekani kwenye elimu hasa govt. schools. Ila ingeboresha kwa wakuu na waratibu elimu kata ingesaidia sana
 
Umeenda chakaa! Wakuu wa shule wengi wao ndio waharibifu wa shule kwa uongozi mbovu hadi watoto wanafeli.
 
Nadhani walimu wakuu ndiyo wakuwajibishwa kwa kila udhaifu na uzembe utakayotokea shuleni kwake kwani yeye ndiyo kapewa dhamana ya kusimamia kila shughuli ndani ya shule yake...Kama kuna mwalimu atimizi wajibu wake hatua za kinidhamu zifutwe na nadhani kama mwalimu huyo hatojirekebisha itafikia mahali atafukuzwa shule kwa kushindwa kutimiza wajibu.
 
Ili kubadili na kupunguza kuporomoka kwa elimu yetu, maamzi yanatakiwa yatolewe juu na walimu wakuu na wakuu wa shule, ili mwalimu akifundisha ajisikiavyo/kizembe kizembe yeye afukuzwe tu bila kusubili mwajiri wake/mkurugenzi, kama ilivyo kwa shule binafsi.
Wakuu wa shule za private wana mamlaka ya kuajiri na kufukuza kwa shule za serikali mkuu wa shule hana tofauti na kilanja au monitor.
 
Walimu wa kike watafukuzwa kazi sana headteacher akitongoza akikataliwa anafukuza madam teacher.

Lazima kuwe na ngazi za juu zaidi ya mwalimu mkuu.
 
Back
Top Bottom