Nkiwa sekondari o level nlipata mwalimu jina la serikali anaitwa Kavishe, lakini jina lake analotamba nalo ni "Red Devil". Huyu alikua mwalim wangu wa darasa.
Siku kama 3 baada ya kuripoti form nyoko, nko na masela tunapiga stori, kumbe darasa iko next to ofisi ya ticha bigi a.k.a mwalim mkuu.
Hyo siku alikua na wageni af mayowe kama yote, akaja chap akamwambia "monta" mmoja kiherehere atoe list ya waungwana wanaopiga mayowe.
Kama kawaida mimi na masela wangu wa back bencher tukatoka mbele kibingwa tukijua hakuna maajabu.
Ile tumetoka nje timepiga magoti kwa mbaaali akaja redi devo.
Mkuu akamwambia, unaona wanao? Wananipigia makelele embu deal nao.
Jamaa akatuchekiii, af akasema subr nakuja. Akaenda ofisini akarudi na mzigo wa kuni.
Akaanza kutembeza kichapo.
Yule fala anachapa sijawahi ona.
Nakumbuka aliniwasha stiki nkaomba poo kwanza. Nkamwambia, aiseee ticha subr kwanza nipumzike hali si hali.
Akadeal na wengine af akaniita, we msanii, unadhani nmekusahau? Kuja hapa senzi sana.
Nkaenda nkamalizia dozi yangu tukarudi klanga lakn maumiv yake sijawahi kusahau.
Sema nin, all in all na kasoro zake alikua na upendo mkuu. Tukienda shamba, tukishamaliza ekari zetu, hakuna kusaidia darasa lolote. Hata aje mkuu kuomba tikawasaide wengine, redi devo yeye anaweka msimamo, "watoto wangu wamemaliza shamba lao lote. Hakuna kusaidia wengine".
Kwaio sisi mapeeeema tinarudi skuli kuiba maji na chakula.
Mungu ampe maisha marefu japo ile Geography yake sikuwahi kuelewa hata chembe nlipita tu kwa kudra za bwana Jesus.