Walimu waitunishia misuli serikali

Walimu waitunishia misuli serikali

IZENGOB

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2014
Posts
323
Reaction score
317
Wakati Ikulu ikikana Rais Jakaya Kikwete kuagiza watumishi wa serikali kuchangishwa fedha, Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kimepinga walimu kukatwa mishahara kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa maabara za shule za sekondari.

Katika tamko lake, CWT imewaonya wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kujiandaa kukabiliana na mkono wa sheria wasipositisha zoezi la kuwakata walimu mishahara yao kwa ajili hiyo na kuwataka kurejesha mara moja fedha zote walizozikata, kabla hawajadaiwa kuzirejesha na faida.

Naibu Katibu Mkuu wa CWT, Ezekiah Oluoch, alisema hayo alipozungumza na NIPASHE baada ya kuulizwa msimamo wa chama chao kufuatia taarifa ya baadhi ya halmashauri kuwakata fedha walimu kwa ajili ya ujenzi wa maabara.

Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Mahusiano Kazini ya Mwaka 2008, mwajiri haruhusiwi kukata mshahara wa mwajiriwa."Isipokuwa kwa ridhaa ya mwajiriwa au kwa matakwa ya kisheria kama vile amri ya mahakama," alisema.

Alisema anatoa salamu hizo kwa wakurugenzi wote baada ya kuwa amepata barua iliyoandikwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, mkoani Dodoma, ikiwaeleza kukata mishahara ya walimu.

Oluoch alisema barua hiyo ilielekeza walimu kukatwa kati ya Sh. 30,000 na 60,000 kutoka kwenye mishahara ya Septemba na Oktoba, mwaka huu, kwa ajili ya utekelezaji wa agizo la Rais la ujenzi wa maabara.

Alisema kwa mujibu wa barua hiyo, makato hayo yanafanyika ili kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete kwa wakurugenzi na wakuu wa wilaya la kuhakikisha wanajenga maabara katika shule zote za sekondari zilizo katika maeneo yao.

"Ndiyo maana baada ya kuipata barua hiyo tumepanga kwanza kuiandikia Ikulu, kwa Katibu Mkuu Kiongozi, ambaye ndiye mkuu wa utumishi serikalini ili kupata ukweli wa maagizo hayo ya kukata mishahara ya walimu," alisema Oluoch.

Alisema haiwezekani walimu wakawa wahanga wa maamuzi yasiyo sahihi ya wakurugenzi na hasa ikichukuliwa kuwa wanalipa Kodi ya Mapato (Paye) na kuwa shule zinazotakiwa kujengwa maabara ni za wananchi.

Oluoch alisema kadhia hiyo dhidi ya walimu inatokea sasa wakati tayari wakiwa na hukumu iliyotolewa na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi mkoani Mbeya ya mwaka 2013 iliyoharamisha maamuzi kama hayo.

Alisema mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Mbozi aliwakata walimu fedha kutoka kwenye mishahara yao kwa ajili ya kuchangia mbio za mwenge na CWT ilimpeleka kwenye tume hiyo.

Oluoch alisema baada ya kusikiliza shauri hilo, tume ilimhukumu mkurugenzi kuwalipa walimu fedha zote walizokatwa na hivyo ikawa hasara kwa serikali.

"Ninavyojua mimi, agizo la Rais halikuwa kujenga maabara kwa kukata walimu mishahara yao. Liliwaagiza wakurugenzi hawa watafute fedha kutoka kwenye vyanzo vyao vingi walivyonavyo na si kwa walimu," alisema Oluoch.

Alisema ikiwa ufafanuzi wa Ikulu wanakoanzia hautawaridhisha na ikiwa zoezi hilo halitasitishwa na walimu kurudishiwa fedha zao, basi watafungua shauri kwenye tume hiyo mkoani Dodoma iliko wilaya ya Kongwa.

Katika toleo letu la jana, tuliandika habari ukurasa wa mbele iliyokuwa na kichwa kisemacho: "Watumishi wa umma wachangishwa fedha za ujenzi wa maabara".

Habari hiyo ilieleza kuwa serikali imebuni utaratibu wa kuchangisha fedha za ujenzi wa maabara kwa kuwachangisha walimu na watumishi wengine wa umma.

Habari hiyo ilinukuu barua ya Septemba 15, mwaka huu, kutoka kwa moja ya halmashauri nchini kwenda kwa waratibu wa elimu wa kata, ikiwa na kichwa cha habari ‘Michango ya maendeleo kuchangia ujenzi wa maabara.'

Ilikuwa inawataka waratibu hao kukusanya fedha hizo kutoka kwa walimu ikitaja viwango vya uchangiaji kuwa ni sh. 60,000 (waratibu elimu kata), Sh. 60,000 (walimu ngazi ya mshahara TGTS F-G), Sh. 30,000 (ngazi ya mshahara TGTS D-E) na Sh. 20,000 (TGTS B-C).

WAZIRI MAJALIWA
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-Tamisemi (Elimu), Kassim Majaliwa, alisema hana taarifa za kusambazwa kwa barua kwa waratibu elimu wa kata, zinazowataka wakusanye michango ya ujenzi wa maabara maeneo mbalimbali nchini na kwamba iwapo kuna michango kama hiyo, suala hilo ni la hiyari na siyo lazima.

"Sina taarifa hiyo. Je, halmashauri gani? Hakuna michango ya aina hiyo kuwa ni lazima. Michango yote kwa ujenzi wa shule zetu ni maamuzi ya wananchi wenyewe. Michango yote ni hiyari," alisema Majaliwa.

BARUA YATHIBITISHA
Hata hivyo, suala hilo linathibitishwa na barua kutoka moja ya halmashauri nchini iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwenda kwa waratibu elimu wa kata yenye kichwa cha habari cha "Michango ya maendeleo kuchangia ujenzi wa maabara" ikiwataka waratibu hao kukusanya michango hiyo.

Barua hiyo, ambayo NIPASHE imeona nakala yake inaeleza kuwa kulingana na agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya ukamilishwaji wa maabara katika shule zote za sekondari nchini, uongozi wa halmashauri umeridhia uchangiaji huo.

Barua hiyo imeainisha viwango vya uchangiaji kuwa ni Sh. 60,000 (waratibu elimu kata), 60,000 ( walimu ngazi ya mshahara TGTS (F-G), Sh. 30,000 (ngazi ya mshahara TGTS D-E) na Sh. 20,000 ( TGTS B-C).

Barua hiyo ya Septemba 15, mwaka huu, imetaka michango hiyo kutolewa kwa awamu mbili; Septemba na Oktoba, mwaka huu na kuagiza walimu wakuu kusimamia michango hiyo kwa shule zao na kuwasilisha fedha hizo halmashauri.

Rais wa CWT, Gratian Mukoba, alithibitisha kupokea malalamiko kutoka kwa walimu juu ya michango hiyo na kusema inapaswa kuwa ya hiari na siyo lazima.
Alisema hiyo ni kutokana na makato ya kisheria kuwa wazi na kwamba, wamewaagiza viongozi wa chama hicho kwenye wilaya kufuatilia na kuhakikisha walimu wanafanya kwa hiari yao.

WAZIRI KOMBANI
Hata hivyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Celina Kombani, alivyopigiwa simu yake iliita bila kupokelewa na hata alivyotumiwa ujumbe mfupi wa mkononi haukujibiwa.

IKULU
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, amesema siyo kosa kwa mtumishi wa serikali kuchangishwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo kama katika halmashauri husika wamekubaliana kuchangishana.

Alisema hayo alipozungumza jana katika mahojiano na NIPASHE iliyotaka kujua mwongozo wa serikali unaeleza vipi kwa watumishi wa serikali katika kuchangishwa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Balozi Sefue alisema suala la mtu kuchanga kwa ajili ya miradi ya maendeleo ni hiari yake na siyo lazima.

"Kama wamekaa wenyewe kama halmashauri wakakubaliana kila mtumishi achangie hakuna tatizo kwa sababu suala la kuchangia ni hiari ya mtu na serikali haiamini kama watumishi wanaweza wakachangishwa bila makubaliano," alisema.

Alisema Rais hajawahi kutoa agizo lolote kwamba, watumishi wa serikali wawe wanachangishwa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

"Mimi sijui kama kweli kuna taarifa kwamba, Rais alishawahi kutoa agizo kwamba, watumishi wawe wanachangishwa fedha. Kama kuna watu wanasema hayo, waeleze Rais alitoa agizo hilo wapi," alisema.


SOURCE:
NIPASHE
 
Hii kweli nimeipenda, hawa wakurugenzi wamekuwa wakitumia jina la rais kuwa ndo kaagiza kumbe wizi mtupu. na sidhani kama kweli hizo hela zikikatwa zitaelekezwa kwenye ujenzi husika.

Wewe mkurugenzi una moyo gani usiyo kuwa na huruma? walimu wanafanya kazi katika mazingira magumu, walim wanapata mshahara mdongo, walimu wana malimbikizo ya mishahara yao selikarini kwa muda mrefuf, walimu ucheleweshwa kupata mshahara, na hivyo maisha yao uwa magum, leo hii ina andika kijibarua chako cha kuwa kata mshahara kwa lazima. utapata laana za bure. au kwa kuwa sisi walimu hatuja kusema wizi wako ndo maana
una amua kututolea makamasi makali yaletayo mafua? mwizi mkuu.


WALIM MSIKUBALI KABISA KWA WIZI HUU.
 
Walimu wa nchi wanataabika sijapata kuona. Hivi kwanini hamna huruma na mtendakazi huyu?? amekosa nini?? kwanini mwalimu tuu?? wewe mkurugenzi bila mwalimu ungekuwa hapo ulipo?? JAMANI HEBU IFIKE MAHALI KUWA NA FANI YA UALIMU ISIWE DHAMBI KHA!
 
Walimu wa nchi wanataabika sijapata kuona. Hivi kwanini hamna huruma na mtendakazi huyu?? amekosa nini?? kwanini mwalimu tuu?? wewe mkurugenzi bila mwalimu ungekuwa hapo ulipo?? JAMANI HEBU IFIKE MAHALI KUWA NA FANI YA UALIMU ISIWE DHAMBI KHA!

Mimi nimesoma bed lakin siwezi kua mwalimu Ng'ooo bola niwe na miradi yangu tu ualimu bongo hakuna nshuu kila onevu walimu tu bana akaaa
 
Walimu wa nchi wanataabika sijapata kuona. Hivi kwanini hamna huruma na mtendakazi huyu?? amekosa nini?? kwanini mwalimu tuu?? wewe mkurugenzi bila mwalimu ungekuwa hapo ulipo?? JAMANI HEBU IFIKE MAHALI KUWA NA FANI YA UALIMU ISIWE DHAMBI KHA!

Mimi nimesoma bed lakin siwezi kua mwalimu Ng'ooo bola niwe na miradi yangu tu ualimu bongo hakuna nshuu kila onevu walimu tu bana akaaa kwa tz ukitaka kua na maisha ya dharau.dhurumiwa nk katika utumishi wa uma kua Mwalimu richa ya one yako form six na first class yako chuo au diploma nzuriiii
 
Walimu wa nchi wanataabika sijapata kuona. Hivi kwanini hamna huruma na mtendakazi huyu?? amekosa nini?? kwanini mwalimu tuu?? wewe mkurugenzi bila mwalimu ungekuwa hapo ulipo?? JAMANI HEBU IFIKE MAHALI KUWA NA FANI YA UALIMU ISIWE DHAMBI KHA!


Ukisikia kuwa nguruwe alimla mwenye shamba ndiyo kama hivi, wanasomeshwa na walimu halafu wanawageuka na kuwafanya vikaragosi wao
 
Sio kongwa tuu..kigoma nao wameamrishwa watoe... huu ni ujinga..hela wanazotumia kulipa wajumbe wa BMK ambalo ni hopeless wajengee hizo maabara
 

Attachments

  • 1412181480808.jpg
    1412181480808.jpg
    79.2 KB · Views: 135
  • 1412181503370.jpg
    1412181503370.jpg
    54.5 KB · Views: 116
Ukisikia kuwa nguruwe alimla mwenye shamba ndiyo kama hivi, wanasomeshwa na walimu halafu wanawageuka na kuwafanya vikaragosi wao

wala siwaonei huruma kwakuwa hawajiurumii.
 
wala siwaonei huruma kwakuwa hawajiurumii.


Huwa sielewi ni kwanini walimu wengi wamekuwa hawajihurumii hata wao wenyewe, au ni kwasababu kuna kipindi wengi walipata nafasi za kusomea hiyo fani wakiwa na alama za chini sana kwahiyo wanairejeshea serikali fadhila! au ni woga kutokana na vitisho vya mabosi wao maana juzijuzi tulisikia wamechangishwa michango ya mwenge kwa lazima, ikawa kama haitoshi wakaambiwa waende kwenye mkesha wa mwenge (kama sijakosea hili lilitajwa kutokea maeneo ya Vikindu au Mkuranga) bila kufikiria siku ya pili wangefundishaje bila kuandaa masomo halafu uchovu + usingizi, kwakweli hawa watu wanahitaji kusaidiwa kwa lazima sasa, maana kama wao wenyewe wameshindwa madhala yake yatakwenda kwa watoto wetu.
 
Back
Top Bottom