Walimu wahamishia familia kwa mmliki wa sekondari

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
Walimu wahamishia familia kwa mmliki wa sekondari Send to a friend Friday, 07 January 2011 20:09 0diggsdigg

Hemed Athuman (TSJ)
WALIMU wa Sekondari ya Mkandawile na familia zao, wameweka kambi nyumbani kwa mmiliki wa shule hiyo kwa karibu wiki mbili sasa kushinikiza kulipwa mishahara yao.

Mmiliki wa shule hiyo, Alfan Mkandawile, anadaiwa kutokomea kusikojulikana baada ya Benki ya CRDB ambayo alimkopesha Sh500 milioni, kuamua kushikilia sekondari hiyo baada ya kushindwa kulipa deni kwa muda uliotakiwa.
Mwalimu wa somo la kiingereza shuleni hapo, Laurent Oyaro, alisema wamelazimika kuhamishia familia zao kwa mmiliki wa shule, ili kujua hatma ya malimbilizo ya mishahara yao.

“Tulikuwa familia za walimu sita tuliohamia nyumbani kwa Mkandawile, lakini tumebaki wawili kwa kuwa wenzetu walishindwa kuvumilia njaa na kuamua kuondoka,” alisema Oyaro. Oyaro aliomba serikali kuingilia kati mgogoro huo, ili kuwaokoa na hali ngumu inayowakabili.

Wanafunzi katika sekondari hiyo ambayo imeanzishwa miaka saba iliyopita, wamebaki njiapanda. Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba wanaoathirika zaidi ni kidato cha sita, ambao kwa sasa walikuwa kwenye maandalizi ya mtihani wa taifa mwezi ujao.
Mmoja wa wanafunzi hao, Mussa Pastory, alisema wanaishi kwenye mazingira magumu, chakula kupatikana ni shida na mpaka sasa wamekwama na kukata tamaa.


source:mwananchi
 
Huyo mwandishi wa TSJ na wewe Ivuga vipi ? shule iko wapi ? Mkoa gani,Wilaya gani ?????
 
wazungu wameanzisha hii kitu ili kuepusha maswali kama swali lako.''google.com''

Pamoja na utetezi wako inabidi ukubaliane na mimi sio uandishi mzuri,sehemu ya tukio ni kiungo muhimu kwenye habari yeyote.
 
Huyu mkandawile si aliwahi kuwa maarufu kwa ufundishaji wa tution Dar.
 
Back
Top Bottom