Walimu wafanyishwa mtihani Darasa la VII

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
PAMOJA na kusoma na kuhitimu madarasa ya juu kuliko wanafunzi wao, imeonekana kuwapo haja kwa walimu wa shule za msingi kupimwa welewa wa masomo wanayofundisha.

Ili kulitekeleza hilo na kupata kipimo halisi cha walimu, Serikali itafanya jaribio la kuwafanyisha mtihani utakaokuwa umefanywa na wanafunzi wao wa darasa la saba.

Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa na kusababisha walimu kushtuka na baadhi yao kuguna, hata hivyo waziri akaendelea kufafganua lengo la kutaka kufanya hivyo.

Alisema masomo ambayo walimu watatahiniwa ni ya Kiingereza na Hisabati, mtihani utakaokuwa umefanywa na wanafunzi wa darasa la saba.

“Lengo ni kutaka kuona kama walimu wa shulezamsingi ni mahiri kuliko walimu wao kwenye amsomo hayo,” alifafnua Waziri.

Kwa muda mrefu Baraza la Taifa la Mitihani(Necta) kwenye taarifa zake limekuwa likitaja Kiingereza na Hisabati kuwa masomo yanayofanywa vibaya na wanafunzi kuliko masomo mengine.

Ufaulu wa masomo hayo kila mwaka umekuwa unashuka hali inayolalamikiwa na wadau kuwa yawezekana uwezo wa walimu wa kuyafundisha ni mdogo.

Waziri aliku wa akizindua Mpango wa Mafunzo ya Walimu Kazini kwa Elimu ya Msingi (MWAKEM), ambayo yatakuwa yakitolewa ngazi ya shule. Mafunzo hayo kwa kuanzia yatahusu Kiingereza na Hisabati.

Dk Kawambwa alisisitiza akisema: “Mimi kama Waziri kuna siku wanafunzi wa darasa la saba wakimaliza mtihani wao wa kuhitimu elimu ya msingi kwa masomo haya, nami nitawaita walimu wa shule husika ili wafanye mtihani huo huo tuone kama uwezo wa walimu wetu ni mkubwa.”

Alisema walimu wanatakiwa kujiongezea zaidi maarifa, hivyo wanoe zaidi ‘silaha’ zao ili wawe mahiri katika ufundishaji wa Hisabati na Kiingereza, hali itakayowafanya pia wanafunzi kufanya vizuri katika mitihani yao.

Awali, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Khamis Dihenga, alikiri kuwa Kiingereza na Hisabati yamekuwa pia tatizo kwa walimu kufundisha na kujifunza na ndiyo maana wameyapa kipaumbele katika MWAKEM.

Mafunzo hayo ya walimu kazini yatakuwa yanatolewa kwa njia ya elimu masafa katika ngazi ya shule kupitia moduli za masomo yanayofundishwa shule za msingi. Walimu wataongezwa moduli ya ujuzi ili waweze kufundisha kwa umahiri.

Profesa Dihenga katika hotuba yake iliyosomwa na Naibu Katibu Mkuu Selestin Gesimba, alisema moduli hizo zinachukua nafasi ya mwezeshaji, ambapo mwalimu atasoma na kupima maendeleo yake mwenyewe kupitia kazi zilizoanishwa.

Alisema wizara imekamilisha moduli za mafunzo kwa masomo hayo, likiwamo la ujuzi ambao ni mahsusi kwa kufundisha umahiri wa mwalimu. Mpango huo kwa sasa uko katika wilaya saba za Hai, Siha, Mtwara Vijijini, Makete, Temeke, Bagamoyo na Magu.

Walimu 2,052 wa halmashauri wameelimishwa huku wawezeshaji 60 wa ngazi ya shule na 42 ngazi ya klasta, wamepewa mafunzo ya kina kwa ajili ya kutoa msaada wa kitaalamu kwa walimu inapohitajika.

Akizindua mpango huo, Dk Kawambwa aliuelezea kuwa na faida kubwa kwani walimu wataunda jumuiya ya wanataaluma, ili kuimarisha ujuzi wao na weledi katika kufundisha na utawafikia walimu wote kwa pamoja.

Alihimiza walimu kutumia kikamilifu moduli za mafunzo ili kuleta matokeo mazuri katika mchakato wa kufundisha na kujifunza kama ilivyokusudiwa, ili kuinua ubora wa elimu nchini.

“Hii ni fursa muhimu kwa walimu kujenga uwezo wao wa kumudu changamoto za ufundishaji na kujifunza katika masomo haya,” alisema Dk Kawambwa.

Naye Naibu Waziri wa Tamisemi (Elimu), Kassim Majaliwa, alizitaka halmashauri za wilaya kuhakikisha zinatenga bajeti kwa ajili ya mafunzo hayo, ili walimu wengi wapate kufaidika.

Alisema wizara yake itausimamia mpango huo kuhakikisha unakuwa wenye mafanikio.

Alisema halmashauri za wilaya na manispaa, zina jukumu la kutumia fedha zao kutoka vyanzo vya ndani na kuhakikisha fedha za kutosha zinatengwa, ili mpango huo upanuke kutoka wilaya saba za sasa hadi nchi nzima.
 
Back
Top Bottom