Walimu wa UPE wapewe tuzo

shikulaushinye

JF-Expert Member
Aug 29, 2014
828
456
Wana jamii inasikitisha kuona kila kukicha hawa walimu walioitwa wa UPE wanadhaulika sana, walimu wa kizazi kile nafikiri bado baadhi wapo mashuleni japo kwa asilimia ndogo kwaani wengi wamestaafu kwa mujibu wa sheria za utumishi umma. Lakini napenda kueleza kuwa haijawahi kutokea na haitatokea Tanzania tukapata walimu wenye weledi na nidhamu ya utumishi kama wale tunao wadhihaki. Me nimebahatika kufundishwa na asilimia 80 ya walimu hawa nikiwa primary. Wachache sana walikuwa na elimu ya kidato cha nne. Nakumbuka katika shule yenye walimu kama 30 walimu wenye elimu ya kidato cha nne walikuwa 4 tu wengine waliobaki walikuwa STD 7 na STD 8 ya zamanni waliopata mafunzo/kozi ndefu na fupi. Walimu hawa walikuwa na weledi mkubwa sana katika kufundisha, walijituma na kujitoa. Wanafunzi tulikuwa na nidhamu ya hali ya juu tofauti na sasa, tulikuwa na uelewa mkubwa sana tofauti na sasa. Sidhani kama STD 7 wa sasa anaweza kwenda kozi fupi akarudi kufundisha wenzake na wakafaulu masomo ya sekondari? STD 7 wa sasa hata kupika chakula cha nyumbani hawawezi.

MAPROFESA WALIOZALISHWA NA STD SEVEN (7):

Maprofesa wote wenye umri wa chini ya miaka 55 kama akina Profesa Mkumbo, Prof Ndalichako na nk. Walifundishwa na walimu hawa tunaowadharau leo, mfano Prof Ndalichako kama sijakosea hata mama yake mzazi alikuwa Mwalimu, lakini nafikiri vijana wanaoendeleza dharau kwa walimu hawa ni vijana wa kizazi cha mkapa na JK maarufu kama school bus, hawajui hata mchaka mchaka au kupiga namba. Leo hii walimu wengi tunaowaita form 4 jioni ni madereva wa BODA BODA elimu itapanda wapi hapo. Elimu hujengwa na nidhamu kati ya Mwalimu na Mwanafunzi. Zamani ukikutana na Mwl mtaani unafikiria utaanzaje kujitetea shuleni kwa mazingira aliyokukuta nayo. Lakini siku hizi mwalimu anamebeba mwanafunzi kwenye boda boda kama mteja. Ukweli walimu wangu wa Primary nitawakumbuka sana, walikuwa na uwezo wa kutunga nyimbo zenye maana, tulifundishwa ngoma za utamaduni, ngojera, kutunga mashairi, kujiamini na nk. Mfano nilipo maliza darasa la saba nilisafiri kwa treni mpaka Dodoma nilipochaguliwa kidato cha kwanza bila kusindikizwa na mzazi wala ndugu, nilipofika shule nililipoti na kununua baadhi ya mahitaji. Lakini watoto wa siku hizi hata wa kidato cha nne ambao ndiyo tunawategemea kuwa walimu wakichaguliwa kidato tano bila kupelekwa na wazazi hawawezi kusafiri kutoka DAR kwenda kuripoti shuleni Musoma.

MWISHO: TUWAPE HESHIMA STAHILI WALIMU HAWA

Tuache maneno ya kejeli kwa walimu hawa, wengi wana uelewa mkubwa kuliko hata maprofesa ambao wameshindwa kusaidia kuliinua taaifa letu kutoka kwenye lindi la umaskini, hawafanyi tafiti za kimaendeleo zaidi ya kufanya tafiti za kutafuta kupanda kuwa maprofesa. Mfano ukienda pale Morogoro maprofesa wengi wamefungua migahawa na Bar. Utasikia hii ni BAR ya profesa Kambarage, Hotel 88 ya Prof Mbiha, sijui LUKILI HOTEL ya prof nani na nk….. wengine wamefuga kuku ya mayai wakati hata uprofesa wake ni wa misitu na nk. Sitaki kuwataja kwa majina lkn orodha ni ndefu sana. Maprofesa wengine wamestaafu bila hata kutunga kitabu kimoja zaidi ya kuandika paper za kupatia udaktari na uprofesa. Wakishapata uprofesa wanageuka kuwa wana siasa na wajasiliamali. Utasikia Prof. Mbunge wa jimbo .. . wenzetu nchi zilizo endelea mapropfesa ni watu wa kufanya tafiti mbalimbali na kuishauri serikali, hapa kwetu wanasubiri eti mpaka Rais awateua, atateua wangapi? Vyuo vikuu vipo vingapi? Tungeni hata vitabu serikali itasoma na kufanyia kazi: akina Prof. Maghembe, Prof Msolwa, Prof Tibaijuka, Prof. Mbalawa, na n.k tangu waingie kwenye siasa wana habari ya kufanya utafiti au kutunga vitabu?
 
Sio tatizo la profesa kuwa mjasiriamali vinginevyo hoja yako imekosa mantiki
 
Back
Top Bottom