Walimu wa Tanzania punguzeni unyonge

njundelekajo

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
310
227
Yule wa msoga aliulizwa unatuachaje huyu unatuanzaje!!!

Kilichokosekana kwa walimu ni UMOJA na UJASIRI tu wa kujipigania

. UMUHIMU na IDADI ya walimu ni sababu tosha na kubwa ya kusikilizwa bila mabango haya!!

Mpaka 15/5/2015 idadi ya walimu wanaofundisha shule za serikali walikua 301,960 wakiwa wanafundisha zaidi ya wanafunzi ml 10..sekondar wanafunzi 1,804,056 na msingi wanafunzi milion 8.23(hotuba ya rais wiki ya elimu 15/5/2015-Dodoma)

Kupitia idadi yenu na wanafunzi mnaowafundisha mnaweza "kusikilizwa" na mashemeji hao mkiamua bila kuisubiri mei mosi na mabango ya aina hii!!
Nguzo Noel .R.
 

Attachments

  • FB_IMG_1462138954402.jpg
    FB_IMG_1462138954402.jpg
    41.7 KB · Views: 58
Walimu ni watu mhimu sana na kila mtu hasa mwanaume anayehitaji mke mara nyingi hupenda kuoa mwalimu! angalia jk na magufuli na pia kuna wagu wengi wameo walimu.

Kwa sasa walimu wamekuwa kero katika taifa hili kila ukigusa wapo! sasa imekuwa fasion ya kulia lia kila may mosi bila maamzi sahihi! MARA SHEMEJI UTATUACHAJE! ilikuwa kwa JK sasa kwa Magufuli.

Ukiangalia historia ya nchi hii hata baba wa taifa alikuwa mwalimu lakini bado hali yao inakuwa mbaya kimaisha pamoja na viongozi wa nchi kuwa na wake walimu na hata kuwa na rais mwalimu bado walimu ni kulia kila siku.

Je, ni kweli salma kikwete hakumwambia JK matatizo ya walimu na je ni kweli mama janeth hajamwambia Magufuli mahitaji ya walimu na je ni kweli Magufuli au jk hawakuyajua au hawajui mahitaji ya walimu.

Walimu nchi hii wamebaki kubeba mabango kila may mosi kwa shemeji yao/zao.


Walimu hukumbukwa na serikali kipindi cha uchaguzi tu na hukumbukwa kwa kulipwa vimadeni vyao na kupewa nafasi za kusimamia uchaguzi baada ya hapo wanabaki na hali ile ile!

Walimu wamekuwa watu wa kudanganywa na kudanganyika kirahisi sana.

Makonda naye kawamaliza na nauli bure sijui inaendeleaje!

Siku mkijielewa walimu kuwa mna dhamani kubwa mtachukua maamzi mazuri na siyo kubeba mabango ya shemeji tena!
 
Back
Top Bottom