Walimu wa Sekondari kusimamia Mitihani ya Darasa la 7. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walimu wa Sekondari kusimamia Mitihani ya Darasa la 7.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by kiwatengu, Aug 20, 2012.

 1. kiwatengu

  kiwatengu JF-Expert Member

  #1
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 14,420
  Likes Received: 3,358
  Trophy Points: 280
  Wana JF je, hizi tetesi za walimu wa sekondari kusimamia mitihani ya darasa la saba ni za kweli? na kama ni kweli lengo ni nini?
   
 2. Stanley.

  Stanley. JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 493
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hiyo sio tetesi ni kweli waziri wa Elimu Mh. Kawambwa amelieleza bungeni kupitia kauli za mawaziri. Alisema sasa hivi mitihani ya darasa la saba itakuwa na MSIMAMIZI MKUU ambaye atakuwa mwalimu wa sekondari. Kwa hiyo kutakuwa pia na wasimamizi wadogo kama zamani.
   
 3. samilakadunda

  samilakadunda JF-Expert Member

  #3
  Aug 20, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 1,701
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  lengo lao nn? Hawajamaa wanafanya siasa maisha ya watoto masikini wananikera kiukweli,badala ya kujadili jinsi ya kuongeza walimu na kuboresha shule za kata wanakuja na ujinga wao,unajenga choo wakati hujui utakula nn??
   
 4. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #4
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  hapa ni kuwadharau walimu wa shule ya msingi
   
 5. n

  nkisumuno JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa mawazo hayo finyu kweli uwezo wa kufikiri wa waziri Kawambwa umefika mwisho. Tunaitahadharisha serikali iache kuchezea walimu wa shule za msingi ambao ndiyo waliotufikisha hapa. kama ni hivyo basi wafundishe hao walimu wa shule za sekondari. Walimu wametoka kwenye mgomo hata hawajaisha wanakuja na tamko la kitoto. Huyo Kawambwa kashindwa hata kusimamia miundombinu leo kapewa elimu kweli watanzania tunapelekeshwa.
   
Loading...