WALIMU WA SANAA(ARTS) WATOA MAONI JUU YA DR. JOHN-2020.

Rais2020

JF-Expert Member
Jul 14, 2016
3,248
5,537
Katika hali ya kuonesha uzalendo,walimu waliohitimu masomo ya sanaa( arts) wameelezea furaha na matarajio yao juu ya maamuzi yanayofanywa na awamu ya tano ya mhe. Dr.John Pombe Magufuli. Walimu hao kwa nyakati tofauti wanaishukru serikali kwa kutowaajiri toka wahitimu vyuo na Sababu walizotoa ni hizi hapa:

1. Amewafundisha elimu ya ujasiriamali.
Walimu hao wa masomo ya Sanaa wamepata elimu kubwa sana ya ujasiliamali ambayo inawaingizia kipato kizuri tu ambacho kinawafanya kuweza kumudu maisha ya mtaani pamoja na kuwepo na hali ngumu ys kiuchumi nchini.

2. Amewafundisha kuwa sio lazma kazi uliyosomea ni lazima uifanyie kazi.
Walimu hao wakiwa na nyuso za furaha kabisa wanafurahia kufanya kazi na kupata ujuzi tofauti kutoka kada zingine. "Toka serikal isitishe ajira nimeajiriwa kama mhudumu wa mahakama ya mwanzo ambapo kila siku huwa nasafisha maeneo ya mahakama na kuhakikisha na boresha mazingira ya mahakama hii kwa kupanda miti ba kuimwagilia kila siku" mwalimu huyo alinena huku akifurahia kabisa kazi hyo huku akiwataka walimu wenzake waache kulialia juu ya ajira.

Matarajio ya walimu
Walimu hao walinieleza mambo mengi sana na kusema kuwa wanamuomba mhe. Dr.John aendelee kukazaa uzi ili hata watakaomaliza mwakani waweze pia kupata elimu hii adimu inayotokana na kutokuwepo kwa ajira hizo.

Mwalimu mmoja ambae hakutaja jina lake akiwa na furaha kabambe alisema kuwa mwaka 2020 kura yake itaenda kwa Dr.John ili aendelee kuinyoosha nchi na kuwafanya vijana sasa kufikiria nje ya fani zao.

Hayo ni maoni ya walimu wa Sanaa ambao wanasubiri ajira. Je, yapi maoni na mawazo yako juu ya uraisi 2020??
Nawasilisha.
Rais2020
Rais wa mioyo ya watu.
Rais atakayefanya muishi kama malaika.
 
Maneno mazuri sana kutoka kwa vijana wenye guraha.
[HASHTAG]#tukutane[/HASHTAG] 2020
 
Nimeupenda uwasilishaji wako wa mada.

By the way mimi napita tu naelekea kujunua Luku ya mwaka mzima kabla tamko la Muhongo halijatenguliwa
 
Back
Top Bottom