Evelyn Salt
Platinum Member
- Jan 5, 2012
- 77,672
- 167,738
Poleni na majukumu walimu, najua kazi yenu ni ngumu sana kumfundisha mtoto namna ya kushika penseli hadi kuja kujua kusoma sio swala dogo, hapo ndipo msingi wa elimu ulipo kama msingi utakosewa kifuatacho katika level za juu hata nyie mnakifahamu.
ila kuna tabia mnayoifanya kwa watoto sio haki hata kidogo huenda mnafanya ili kuwaaminisha wazazi kuwa mnatoa elimu nzuri kwa watoto na kuvutia biashara yenu, tafadhalini walimu kwa hilo mnabomoa hamfurahishi wazazi bali mnaharibu watoto....acheni tabia ya kuandikia watoto wafundisheni, wajengeeni uwezo wa wao kujua kuadika.
haiwezekani daftari la mtoto limejaa ma excellent tuuu, kafundshwa a-z lakini hata a hawezi kuisoma wala kuiandika na hapo kwenye daftari kuna mwandiko mzuri kwelikweli kafundishwa 1-10 lakini kuhesabu 1 hadi 5 hawezi...acheni wazazi watambue uwezo halisi wa watoto wao ili wapate namna ya kuwasaidia zaidi mfano kwa wale ambao ni slow learners, kuliko kutoa matokeo fekero kila mtihani mnajaza 90% wakati sio uwezo halisi wa mtoto.
Wakati wa mitihani ndio haswaaa mnawaandikia tena kwa miandiko mibaya ili ionekane ni mwandiko wa mtoto, sio sawa kwa hili acheni hii tabia.
Madame. ES