Uchaguzi 2020 Walimu wa masomo ya Sanaa (Arts) walionyimwa ajira tangu 2015 hadi 2020 tutampigia kura Tundu Lissu

MANYORI Jr

JF-Expert Member
Mar 25, 2012
462
343
Ndugu wanajukwaa wasalaam,

Kama kichwa cha uzi kinavyosomeka ninahakika unayesoma uzi huu unafahamu kwanini umeufungua ili uusome.

Kwa muda wote ambao serikali ya awamu ya tano imekuwa madarakani, suala la ajira limegeuka kuwa giza lililo gizani hasa ajira za kada ya ualimu ambayo kwa kiasi kikubwa ndimo walimo watoto wa Ma'Kajamba nani na Mzee Tokomea.

Sambamba na hili, ajira za ualimu masomo ya sanaa hasa kwa wahitimu wa shahada('Digrii') kwa awamu yote ya serikali hii hazipo na zimesahaurika kabisa!

Vijana ambao kwa jasho na damu wamesotea digrii hizi wamekosa haki ya kuajiriwa kama walimu wengine wanaopewa fursa zenye upendeleo kwa kigezo cha uongo cha uhaba!

Serikali hii inahimiza wanafunzi na walimu watumie Lugha ya Kiingereza bila kuwa na Walimu waliosomea kufundisha Lugha hii adhimu na mawasiliaono ya kidunia.

Serikali hii imekuwa ikijinasibu kuitukuza historia bila kuwa na walimu wa somo la History mashuleni ambako ndiko kwa nyakanga mkuu.

Serikali hii imekuwa ikijitia kukihusudu Kiswahili kama ishara ya kukienzi na kukitukuza na kufikia kiasi cha mkuu wa mashetani kusema ni uzalendo huku shule zikiwa hazina kabisa walimu wa somo la Kiswahili.

Serikali hii imekuwa ikiwataka raia kuwa wema na waadilifu kwa jamii kwa kuzilinda mila na desturi zenye tija kwa jamii huku ikifahamu vyema kuwa hapana walimu wa somo la uraia shule nyingi za sekondari.

Ni kwa misingi hii ya unafiki serikali hii imeharalisha kuwanyima ajira walimu wote waliohitimu digrii masomo ya sanaa katika awamu yake yote.

Vijana hawa wamepiga sana kelele juu ya hali hii iliyozika ndoto zao kwa muda wa miaka mitano tangu 2015 na majibu ya watetezi wa wanyonge ni kuwa WAJIAJIRI!

SISI WALIMU WA MASOMO YA SANAA TULIONYIMWA AJIRA TANGU MWAKA 2015 HADI 2020 TUNATAMKA KWAMBA; KURA JIPIGIENI!

SISI TUNAMUUNGA MKONO MH. TUNDU LISSU NA TUTAMCHAGUA AWE RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ASUBUHI JUMATANO TAREHE 28 MWEZI WA 10 MWAKA 2020 KWA UHURU, HAKI NA MAENDELEO YA WATU.

MBIO ZA SAKAFUNI HUISHIA UKINGONI NA MGUU USHAOTA TENDE.

Imetolewa na Walimu Masomo ya Sanaa Wasio na Ajira Tanzania 27/10/2020 saa 18:56_
 
Back
Top Bottom