Walimu tulioajiriwa 2012 Ileje tumewakosea nini serikali? Malimbikizo hatulipwi madaraja hatupandi!

May 4, 2013
91
25
Walimu walioajiriwa 2012 ilibidi wapande madaraja July 2015 lakini haikuwa hivyo, tukaendelea kuchapa kazi.

Sasa namuomba waziri simbachawene atuambie sisi walimu wa Ileje tunadharauliwa au hatufahamiki na serikali?

Wenzetu wilaya zingine wamepanda madaraja tokea mwezi wa kwanza sisi hadi Leo bado.

Tumbua jipu la TSD-Ileje, utumishi-Ileje na mkurugenzi naona wanawakwamisha sana.sSiku ukija Ileje utajionea vizuri.

Tunaomba msitushushe ari ya hapa kazi tu! Ila tunasononeka kazi bila hela mmmmmmmh
 
adui namba moja wa mwalimu ni halmashauri yako hapohapo ulipo. FANYENI KAZI MTAPANDISHWA MWAKA HUU KWANI WENGI TU WALIOAJILIWA 2012 TAYARI MAMBO YAMEIVA TANGU JANUARY 940+
 
Tumieni utaratibi rasmi kufikisha malalamiko yenu kwa Mkurungenzi, asipo yashughulikia, myafikeshe kwa Waziri husika na sio humu Jamiiforums ambapo wengi wanaochati sana humu hata darasa la saba hawajamaliza ndio maana wanajibu kidarasa la sabasaba!
 
Alowambia muajiliwe 2012 nani?
wahitimu form 4 2012 tuliwapa sifuri za kutosha
wamekuwa madada poa saivi tunawakamata mbona hawalalamiki?
 
Ileje ni mojawapo ya ngome za kuaminika za CCM katika mkoa wa Mbeya. Usichokijua mwalimu mleta mada ni kwamba, CCM wanaposhinda kwa kishindo basi ndipo wanapopunguza huduma na kamwe hawajishughulishi na watu wa maeneo hayo katika kusimamia maendeleo yao.

Hali hiyo ilikuwepo katika mikoa ya kusini (Lindi na Mtwara), baadaye wale wamakonde walikuja kushtuka na kupelekea CCM ipigwe kwenye majimbo 7. Leo hii, miezi michache baada ya uchaguzi, serikali imepeleka jumla ya bilioni 50 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara ya lami toka Mtwara mjini kupitia Tandahimba na Newala hadi Masasi. Katika wilaya nyingi hapa Tanzania, walimu walioanza kazi 2012 washapandishwa madaraja.

Walimu wa ngazi ya shahada ambao walikuwa kwenye TGTS D wameshapandishwa daraja tangu mwaka jana na sasa wana-enjoy kamshahara kao basic salary ya Tshs. 940,000 wakiwa katika daraja jipya yaani TGTS E huku wewe ukiendelea kulia na TSD, Murugenzi na Afisa Utumishi. Mjomba endeleeni kushirikiana na Wandali kuichagua CCM, mtafanikiwa tu kama si kuishia kula viwavi jeshi kama wale Wagogo wa Chamwino.
 
Wamechelewesha upandaji wa madaraja kwa walimu na kuisababishia madeni serikali,kushusha ari ya kufanya kazi na kutengeneza chuki dhidi ya serikali na wafanyakazi wake.
 
Back
Top Bottom