Walimu si Muhimu kwa Taifa la Tanzania. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walimu si Muhimu kwa Taifa la Tanzania.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kimboka one, Aug 3, 2012.

 1. k

  kimboka one JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 734
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Serikali kama kawaida yake imeagiza mahakama kusimamisha mgomo wa waalimu na kuwalazimisha warudi kazini kuendelea na mgomo baridi kwa sababu wao wala watoto wao si wahanga wa huu mgomo.

  Ila hawa viongozi wetu wasio na huruma na raia wa nchi hii wajue mwisho wao hauko mbali kuna siku hao watoto wanaomaliza darasa la 12(form 4) na la saba wakiwa hawajui kusoma, watavyamia magorofa yao na kudai kugawana mali walizo wadhulumu,leo wataniona kama mwehu hivi ila ipo siku wa si mbali ambayo viongozi wote watalazimika kutembea na SMG na askari wenye silaa kali kutokana na hasira ya watanzania kwao.

  Mimi sitaki kujadili chochote kutokana na mgomo huu ambao mkuu wa nchi anaona hauna madhara makubwa kwani ‘walimu wakigoma mitaala bado ipo watakuja wengine kufundisha’ hivyo ata wakigoma hakuna madhara.hivyo hatuna pesa za kuwapa waalimu ila za wabunge,mawaziri,maVX ,G8 na magorofa ya vigogo pamoja na posha za kila aina,zenyewe zipo ila za waalimu kwa kuwa si muhimu hazipo!.

  Wadau mi ngoja nitoke tu hapa hii nchi si mahali salama pa kuishi tena!.
   
 2. Asabaya

  Asabaya JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 1,317
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Nichukue na mie unakoenda..
   
 3. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #3
  Aug 4, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,892
  Trophy Points: 280
  Walimu wamezidi ukilaza na woga wewe ukiamua kugoma nenda moja kwa moja kwenye mgomo ni mahakama ipi au serikali ipi itakayokuruhusu kugoma?? mshahara wa walimu nafikiri unawatosha sana ndio maana wametishwa kidogo wakafyata!!
   
 4. A

  African teacher Member

  #4
  Aug 4, 2012
  Joined: Aug 1, 2012
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tumefyata eeeh'goja muonje utamu matokeo yajayo'hapo ndipo utakapojua ka tumefyata
   
Loading...