DALLAI LAMA
JF-Expert Member
- Jan 31, 2012
- 8,652
- 2,642
Hao sio walimu,ni kikundi cha wahuni
Walimu wapi hao, maana walimu wote awapo UKAWA
Katika vuguvugu linalotokea sasa la wanasiasa wakongwe na baadhi yao vijana kushuhudiwa kutangaza nia imewafanya wanataaluma wa kada ya ualimu Mkoa wa Arusha kutumia fursa hiyo kumtaja mtu wanayemtaka.
Nikizungumza nao kwa pamoja walionyesha kuwa na imani ya hali ya juu kwa Mh. Lowassa na baadhi yao walikwenda mbali kwa kutoa takwimu za mambo aliyowahi kuyafanya ambayo yalisaidia kuinua elimu.
Mojawapo likiwa ni ujenzi wa shule za kata 1500 nchi nzima ambapo walidai baadhi yao wanafanya kazi huko.
Pili ni kwamba alipunguza tatizo la ajira kwa kada hiyo maaana shule zote hizo bado hazijapata waalimu wa kutosha hivyo kama sio jitihada zake tatizo la ajira kwa kada hiyo lingekua gumu na endelevu.
Pia waliendelea kusema alipunguza tatizo la watoto wa mitaani kwa kipindi cha miaka miwili tu aliyokaa madarakani akiwa waziri mkuu na ndio maana miaka saba sasa toka astaafu kuna makundi kama panya road,Wamarekani weusi ambavyo ni vya kihalifu na hii ni kutokana na kuwa na watoto wa mitaani na ukosefu wa ajira.
Ukiachilia mbali masuala hayo pia walimsifu kwa utendaji wake na kwa kuwa na maamuzi magumu yasiyo tetereka na mwenye kujiamini achilia mbali misukosuko ya kisiasa aliyopitia ambayo ilipelekea kufanya maamuzi magumu ya kujiuzulu kunusuru chama na Taifa kwa ujumla wake.
Wakienda mbali zaidi walisema hata Kama itawezekana wao watahusika moja kwa moja kumchukulia fomu ya kugombea na kama ni kampeni watahakikisha wanakua nae pamoja kwani wanaamini Tanzania inamuhitaji yeye na so mtu mwingine kwa sasa.
Ikumbukwe kwamba Mwl. Ndiye aliyekuwa mkombozi wa Taifa hili kutoka kwa wakoloni hivyo ni jukumu la waalimu kuendelea kuhakikisha Taifa linakua ndani ya mikono salama.
Hayo yalisema na waalimu wa mkoa wa Arusha wakati wa maadhimisho ya miaka saba tika Mh.Lowassa ajiuzulu wadhifa wa uwaziri mkuu kutokana na makosa ya watendaji wa chini yake.
Nawasilisha
Hao watakuwa walimu wa UPE, tena wale ambao ukiwazawadia vichupi wanaweza kukugeuza Mungu wao
Si kweli kuwa walimu ni UKAWA; wangekuwa huko CCM isingekuwepo madarakani. Walimu wengi ni CCM bwana...!
ndugu takwimu gan ulzotumia? au kutoka chanzo kip cha taarifa?
hiyo taarfa ya kwamba walmu wamesema wapo tayar kumuunga mkono na ikibid kumchukulia fomu ni za kizush na za kupuuzwa.
mwalimu ni mtumish wa umma asiyetakiwa kujiusisha na siasa,labda kupiga kura tu_____na walimu wa sasa si sawa na walimu enz za mwalm____kwa hiyo usitegemee unayofikiria kutoka kwa walim ambapo mlikuwa mnawaburuza mnavyo taka.
Niko nawalimu hapa wanasema hili jungu limepikwa Munduli wamekata huu upuzi wao wapo ukawa wanajuta kitu ccm wanachowafanyia
Bila ubishi Mhe LOWASA ana sifa za kuongoza kitaifa na kimataifa. Mimi naahidi kumtolea milioni moja ya kuchukua fomu ya kugombea URAIS ndani ya chama kubwa CCM
Ww nani kakuambia hawatakiwi kujihusisha na mustakabali wa Nchi hii? Mbona kitila mkumbo ni mtumishi wa Umma pia hapa ni nyadhifa ndio hazitakiwi kwa kuwa kutakua na conflict of interest waalimu wameamka ss wamechoka kulalama wanafanya vitendo