Walimu kuomba wapandishwe madaraja wakati shule zao zimefanya vibaya ni halali?

Status
Not open for further replies.

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
52,003
Kumekuwa na kilio kuwa walimu hawapandishwi madaraja kwa wakati.Kilio hiki kimekuwa kikipelekea wengine hata kuandamana kwenda ofisi za serikali kupeleka madai hayo.

Ukija kuangalia matokeo ya mitihani ya Taifa kwa hao wanaodai kupandishwa madaraja hali mbaya watoto wanakuwa wamefeli hadi basi.

Swali ninalojiuliza hivi kupanda madaraja walimu ni kitu gani huwa kinaangaliwa? Hivi watoto shule wanafeli halafu mwalimu anapanda daraja?????? Hiki si kituko.Nilitarajia ashushwe daraja.Wengi wanaodai hawajapandishwa ukweli ni kuwa hata daraja walilonalo wanatakiwa washushwe.

Nadilchako atusaidie kipimio cha mwalimu kupanda daraja ni nini?
 
kuna mambo 3
1.inawezekana walimu wamejitahidi lakini wanafunzi hawajisomei wenyewe sio kosa la mwal.hapo
2.Inawezekana walimu wamejitahidi lakini serikali haiwawezeshi mazingira mazuri ya wanafunzi kufanya vizuri,mfano shule nyingi zilizofelisha sana ni za serikali ambapo hamna vitabu,laboratories,libraries pamoja na mazingira mabovu kwa walimu

3.Sio lazima wanafunzi wote wafaulu ndo maana kunafanyika mtihani,mfumo wa elimu duniani ni 'pyramid' mnaanza wengi mwisho wamalize na wafaulu wachache
 
Fanya utafiti mzuri ndo uje na bandiko lako! Walimu wanapelekewa watoto sekondari wenye uelewa mdogo sana, wengine kuandika inakuwa shida! Sasa unamtaka mwalimu wa sekondari aanze kufundisha kuhesabu na kuandika?

Madaraja ya walimu kutopandishwa ni jipu linalosubiri kutumbuliwa, haiwezekani mwalimu aliyeajiriwa 2012 mkoa wa Geita apandishwe daraja baada ya miaka 3, lakini mwaka huo huo mwalimu wa kinondoni leo mwaka wa 4 hajapandishwa daraja huu ni ubabaishaji mkubwa sana!
 
kuna mambo 3
1.inawezekana walimu wamejitahidi lakini wanafunzi hawajisomei wenyewe sio kosa la mwal.hapo
2.Inawezekana walimu wamejitahidi lakini serikali haiwawezeshi mazingira mazuri ya wanafunzi kufanya vizuri,mfano shule nyingi zilizofelisha sana ni za serikali ambapo hamna vitabu,laboratories,libraries pamoja na mazingira mabovu kwa walimu

3.Sio lazima wanafunzi wote wafaulu ndo maana kunafanyika mtihani,mfumo wa elimu duniani ni 'pyramid' mnaanza wengi mwisho wamalize na wafaulu wachache

Kwa mfano wewe ndiye unayehusika kupandisha walimu vyeo ungeangalia nini ukitaka kuwapandisha.Kusema mwalimu yule anastahili kupanda cheo ungeangalia kitu gani?
 
Wakati mwingine huwa nasema jf is not fair at all, nilitoa post humu ya kueleza changamoto za walimu, lakini MODS wameifuta labda kwa kuitetea serikali. Leo kuna watu Jingalao na huyu YEHODAYA wanawatukana na kuwaponda walimu wa nchi hii bila ya utafiti wowote jf wameachia mabandiko haya bila woga wala kukemea.
Jf badilikeni, heshima yenu inaporomoka.
 
K
Kwa mfano wewe ndiye unayehusika kupandisha walimu vyeo ungeangalia nini ukitaka kuwapandisha.Kusema mwalimu yule anastahili kupanda cheo ungeangalia kitu gani?
Tatizo la lumumba hamjui walimu wanapata shida gan nchii....hizo shule za kata hata vyoo hazina .....wanafunzi tangu elimu bure ianze ndo hata kula hali ,unawezaje kufundisha mtu mwenye njaa akuelewe ?? Tatizo ni serekali ilijisahau majukumu yake ,elimu inaendeshwa na wanasiasa .....ambao watoti wao hawasomi huko.....
 
  • Thanks
Reactions: ydn
Kufeli na kufaulu ni vitu vya kisayansi vilivyopangwa kwa malengo maalumu,kupandishwa daraja au kushushwa daraja hakuhusiani na mambo hayo.
 
Kufeli na kufaulu ni vitu vya kisayansi vilivyopangwa kwa malengo maalumu,kupandishwa daraja au kushushwa daraja hakuhusiani na mambo hayo.

Kupandishwa madaraja ni kwa kienyeji si kisayansi?
 
Inawezekana kutokupandishwa madaraja nayo ikawa sababu mojawapo ya kutofaulisha. Poorly motivated workers often times underperform. Wapandishwe kisha tupime utendaji wao kihalali.
 
kuna mambo 3
1.inawezekana walimu wamejitahidi lakini wanafunzi hawajisomei wenyewe sio kosa la mwal.hapo
2.Inawezekana walimu wamejitahidi lakini serikali haiwawezeshi mazingira mazuri ya wanafunzi kufanya vizuri,mfano shule nyingi zilizofelisha sana ni za serikali ambapo hamna vitabu,laboratories,libraries pamoja na mazingira mabovu kwa walimu

3.Sio lazima wanafunzi wote wafaulu ndo maana kunafanyika mtihani,mfumo wa elimu duniani ni 'pyramid' mnaanza wengi mwisho wamalize na wafaulu wachache
hivi walimu hawana 'OPRASS'
 
Kwani mukishindwa battle kwenye vita walionusurika na kuuwawa wakirudi hawapandishwi vyeo? Kufanya vibaya kwa shule zao kuna sababu ambazo inatakiwa zijulikanwe na zifanyiwe kazi. Kupandishwa daraja mwalimu inatokana na urefu wa huduma alizotoa katika sekta ya elimu na haina mawiano na utendaji wa shule husika. Sababu kubwa za matokeo mabovu yako nje ya uwezo wake kiutendaji. Kwa mfano, mwalimu hana haki ya kuchaguwa mwanafunzi anayehisi atafanya uzuri katika masomo, shule nyingi za binafsi zinazofanya uzuri, huwezi kuchaguliwa kujiunga nazo mpaka ufanye mitihani yao na mahojiano juu. Tunaona JW na polisi kila siku wanapandishwa vyeo, jee wamefikia malengo yao waliyoekewa? Kupandishwa daraja kwa walimu itafanya wazidishe mapato ambayo itawapa motisha ya kuengeza bidii kwa kuwapunguzia ukali wa maisha ambayo ni changamoto kubwa kuliko zote
 
Kupandishwa madaraja ni kwa kienyeji si kisayansi?
Unajua sheria ya kazi inasemaje kuhusu kupandishwa madaraja na cheo?? Kupanda daraja ni haki ya mtumishi!!
Halafu ni wapi imedhihirika kuwa Walimu ndo chanzo cha wanafunzi kufeli?? Unajua changamoto zinazokabili sekta us Elimu na nani wa kulaumu??
 
mbumbu at work, how much you earn per month for this kind of threads. mwenzako nachukua pesa ndefu sana kwa kufanya kazi kwenye ward school.

wewe unajaa majungu jf usikute hata kazi huna, unaishi kwenu kama ray wa bongo movie.

pole sana yehodaya madaraja tupanda kila baada ya miaka mitatu na mishahara itapanda kila mwezi julai ualimu raha sana Nazi kuandaa lesson na scheme baaaaas mambo mengine baadae
 
Ninavyo fahamu mimi kwauelewa wangu mdogo, nikwamba mfanyakazi yoyote au mtumishi yoyote waserekali anapofanya kazi kwakipindi flani nilazima mshahara wake upande, kwahiyo mwataka walimu wasipandishwe madaraja wapande secta zingine, hiyo nihaki yakila mtumishi msiwa wabague walim wetu.
 
s
OPRASS Walimu wanajaza kila mwaka!! Na Bila kujaza Oprass hupandishwi daraja
sidhani kama kipimo cha utendaji kazi wa mwalimu ni vipindi anavyofundisha bali ni kiwango cha kufaulisha....so inabidi walimu watumie mbinu mbadala badala ya kulalamika...
 
Nadhani ni haki yao,ishu ya kufundisha na kufaulu nadhani wanafunzi wa shule za serikali hawana akili za darasani hasa watoto wa miaka hii
 
s

sidhani kama kipimo cha utendaji kazi wa mwalimu ni vipindi anavyofundisha bali ni kiwango cha kufaulisha....so inabidi walimu watumie mbinu mbadala badala ya kulalamika...
Mwalimu anachangia asilimia 30% katika ufaulu wa wanafunzi 70% zingine ni mwanafunzi, mazingira, malezi, nk nk
 
s

sidhani kama kipimo cha utendaji kazi wa mwalimu ni vipindi anavyofundisha bali ni kiwango cha kufaulisha....so inabidi walimu watumie mbinu mbadala badala ya kulalamika...
Na wapi imekuwa proved kuwa kufeli kwa wanafunzi kumesababishwa na walimu?? Wizara wana tafiti na majibu wanajua source na kamwe hawaangaiki!! Sasa msikimbie majukumu kwa kuwasingizia walimu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom