Walimu kuhama kituo kwa kubadilishana iangaliwe upya

NJALI

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
1,534
1,090
Kuna utaratibu sijui ulianzishwa na nani pia sijui kama ni sheria kwamba mwalimu ili ahame kutoka mkoa, wilaya moja kwenda mkoa, wilaya nyingine anapaswa kutafuta mwalimu wa KUBADILISHANA nae.
Hii sio haki, kuna maeneo nchi hii ukipangiwa kazi unaweza hadi ukastaafu bila kupata MTU wa KUBADILISHANA nae.

USHAURI WANGU
Serikali ingeweka miaka mitatu au mitano tangu mtumishi apangiwe KITUO iwe ruksa kuhama.

Pia mtumishi anaefanyia kazi Halmashauri ya mji, au manispaa au jiji aruhusiwe kuhama kwenda Halmashauri za wilaya bila KUBADILISHANA. Kikwazo kiwekwe MTU kutoka wilaya kwenda jiji, manispaa NA miji hadi atimize miaka Fulani iliyowekwa na serikali.
Karibuni wadau.
 
Ulitumwa usomee ualimu mbona uzungumzii polisi au madaktari
 
Mwalimu kutaka kuhama kwenda anapopataka ni suala moja na serikali kuhakikisha kuna mgawanyo fair wa walimu kwa halmashauri zote ni suala lingine lakini yote yanategemeana. Ukitilia mkazo suala moja utaathiri suala jingine. Masuala kama haya yanasumbua sana sana sana...
 
Back
Top Bottom