Walimu au ndege?

Walimu au ndege?

Kilosaone

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2015
Posts
411
Reaction score
224
Adui wa mwalimu ni mwalimu

Mwalimu ndiye alikuwa kiongozi wa nchi ya Tanzania tofauti na marais wengine wa Malaysia, South Korea, Taiwani, Singapore ambao walitawala kipindi kimoja na Mwalimu. Bahati mbaya nchi hizi zilikuwa nyuma kiuchumi na zilizokuwa zimegawanyika kimakabila na ukanda.

Fursa adhimu nchi hizi viongozi wake waliboresha mtizamo wao dhidi ya mwalimu. Walimu katika nchi mfano Korea ya Kusini hupewa kila kitu ikiwa ni posho ya familia na kusomeshwa watoto wa mwalimu hadi chuo kikuu bure na serikali yaani mwalimu huachwa awaze namna ya kujenga fikra (building education) za wananchi.

Njoo kwetu muasisi wa nchi alimuona mwalimu kama mtu anayestahili kujitolea na kazi yake haina maana kiasi cha kumuacha mwalimu akisononeka kwa uwingi wa majukumu, yaani hadi leo usishangae mwalimu anagombana na wanafunzi kisa hawajanunua ubuyu kwake. Wanaume kutwa na bodaboda, mikopo kila kona yaani huyu mwalimu atujengee watoto wetu ili baadae wawe wabunifu na viongozi bora.

Mjomba mimi naona umejitahidi kununua ndege nyingi kwa maendeleo ya nchi ila uliowakabidhi hawakuandaliwa vizuri wanajua tumbo na ndugu zao ndiyo kila kitu si taifa. Viwanda itakuwa ndoto kwani mwalimu aliyechanganyikiwa zao lake ni waliochanganyikiwa.

Nawasilisha

(NIMEKOPI TOKA GROUP LA WALIMU FACEBOOK)
 
Kwa Tanzania ualimu ni poverty free entry gate, Bora uchome mahindi mtaani kuliko ualimu...
FB_IMG_1572071404943.jpg
 
Nilikua naangalia Fursa Clouds Jana kuna dogo mmoja Arusha alianza hustle zake mapema tangu primary ikafika hatua akawa anakopesha walimu..

Kibongobongo ualimu ni tatizo..wengi waliofanikiwa kwenye ualimu ni wale wabishi na Mara nyingi sio wahudhuriaji wazuri kazini..wanaojiongeza nje ya mfumo.
 
Kulalamika pekee siyo solution, sidhani kama kuna Mwalimu kalazimishwa kuwa kazini.

Ukiona ualimu hauna issue unafanya kitu kingine.

Sidhani kama hayo mataifa yanadahili watu wenye ufaulu hafifu kusomea ualimu kama ilivyokuwa huku.
 
Adui wa mwalimu ni mwalim...

Mwalimu ndiye alikuwa kiongozi wa nchi ya Tanzania tofauti na marais wengine wa Malaysia, South Korea, Taiwani, Singapore ambao walitawala kipindi kimoja na Mwalimu. Bahati mbaya nchi hizi zilikuwa nyuma kiuchumi na zilizokuwa zimegawanyika kimakabila na ukanda.

Fursa adhimu nchi hizi viongozi wake waliboresha mtizamo wao dhidi ya mwalimu. Walimu katika nchi mfano Korea ya Kusini hupewa kila kitu ikiwa ni posho ya familia na kusomeshwa watoto wa mwalimu hadi chuo kikuu bure na serikali yaani mwalim huachwa awaze namna ya kujenga fikra (building education) za wananchi.

Njoo kwetu muasisi wa nchi alimuona mwalimu kama mtu anayestahili kujitolea na kazi yake haina maana kiasi cha kumuacha mwalimu akisononeka kwa uwingi wa majukumu, yaani hadi leo usishangae mwalimu anagombana na wanafunzi kisa hawajanunua ubuyu kwake. Wanaume kutwa na bodaboda, mikopo kila kona yaani huyu mwalimu atujengee watoto wetu ili baadae wawe wabunifu na viongozi bora.

Mjomba mimi naona umejitahidi kununua ndege nyingi kwa maendeleo ya nchi ila uliowakabidhi hawakuandaliwa vizuri wanajua tumbo na ndugu zao ndiyo kila kitu si taifa. Viwanda itakuwa ndoto kwani mwalimu aliyechanganyikiwa zao lake ni waliochanganyikiwa.

Nawasilisha

(NIMEKOPI TOKA GROUP LA WALIMU FACEBOOK)
So sad!!
 
Back
Top Bottom