Click_and_go
JF-Expert Member
- Nov 21, 2010
- 451
- 6
Offcourse watamkumbuka kwa jinsi alivyowatesa kwa miaka 42 kama TZ tunakavyoikumbuka CCM kwa kututesa kwa zaid ya miaka 50. Hiyo ni sehemu ya historia. Hata akina Hitler, Stalin wanakumbukwa......................!!!
Vyovyote iwavyo suluhisho sio hili wanalolitaka wachache wao.Ni kweli watamkumbuka sana. Watamkumbuka kwa kuwatawala kibabe, kujilimbikiazia mali, uwepo wa pengo kubwa la walionacho na wasionacho huku akiwadanganya kwa kuwakambisha kwa uchache rasilimali ya nchi. Watamkumbuka kwa kutaka kuifanya nchi koloni lake (kifalme). Watamkumbuka sana. Lakini pilipili tusiyoila yatuwashia nini? Je nasi tutamkumbuka Mkwere kwa lipi?
Offcourse watamkumbuka kwa jinsi alivyowatesa kwa miaka 42 kama TZ tunakavyoikumbuka CCM kwa kututesa kwa zaid ya miaka 50. Hiyo ni sehemu ya historia. Hata akina Hitler, Stalin wanakumbukwa......................!!!
Hivi ni nchi gani duniani iliyo tamu muda wote?? wana JF twambieni maana libya kila kitu kilikua bure, shule, afya, nyumba na bado Gadaf wamemtoa! Marekani kwenyewe sii kutamu kihivyo!! what type of state do we Africans need?
Hapo kwenye red, kwa wale wanaofahamu world history, tunaye jamaa wa aina hiyo hapa kwetu, a very good speaker, mass puller na ana ushawishi mkubwa (simtaji maana anajijua)!!!
Aliyekudanganya kwamba Libya kila kitu bure nani? Acha uongo...I have been there hamna kitu kama hicho...usipotoshe watu
Youre right, hivi utawala ulioshupaliwa wa gadafi na nchi za magharibi unazidi kwa ubora tawala ngapi mbovu zinzoungwa mkono na kufuata "demokrasia" ya kimagharibi?
Waarabu wakae wakijua wamagharibi hawana rafiki wa kudumu zaidi ya wao kwa wao, wanawatumia waarabu kwasasa sababu wanataka kuwaondoa wale ambao ni tishio kwao na maslahi yao.
Kwa Afrika libya ni moja ya nchi iliyokuwa na uchumi mzuri na maisha ya wananchi kiuchumi yalikuwa yako juu sana kulinganisha nyingine,
Baada ya vugu vugu la Tunisia wamagharibi walitumia mwanya huo kuchagiza vugu vugu hilo kwa wabaya wao wengine, na hatimaye misri wamefanikiwa tayari na nguvu zote zimehamishiwa libya na iran ambapo mambo yamekuwa magumu
DEMOKRASIA inayo mantiki yake ambayo si lazima iwe na tafsiri maarufu ya nchi za Magharibi, kwa kuwa lengo la utawala kwa watawala na watawaliwa mahali popote ni manufaa ambayo watawaliwa wanayatarajia.
Katika nchi za Magharibi, tafsiri maarufu ni ya Abraham Lincoln, Rais wa 16 wa Marekani (Februari 12, 1809 Aprili 15, 1865) aliyesema kuwa demokrasia ni serikali ya watu, iliyoundwa na watu, kwa ajili ya watu.
Hata hivyo maana ya demokrasia kwa watu hao wa Magharibi, haikuwa serikali ya watu, inayotokana na historia yao, hatua yao ya maendeleo ya kijamii na malengo yao.
Kwa kiasi kikubwa tafsiri hiyo ya Magharibi ililenga kuficha walichokusudia, ambacho ni mfumo wa Magharibi kwa ajili ya kuwarithisha watu hata wasio wa Magharibi lakini kwa maslahi ya watu wa Magharibi.
Katika historia ya maendeleo ya binadamu, ambayo kwa kiwango kikubwa iliyowekwa katika
kumbukumbu ni ya watu hao wa Magharibi, demokrasia ilikuwepo na ikabadilika kutokana na historia yao, hatua yao ya maendeleo ya kijamii na malengo yao.
Ndivyo ilivyo kwa Libya, inayo demokrasia ambayo haina maana ni demokrasia isiyobadilika, lakini ni demokrasia iliyopo kwa kiwango cha maendeleo cha nchi hiyo, kilichosababisha kukubalika kwa serikali yake na watu wake,,,,,soma zaidi HabariLeo | Walibya watamkumbuka Gaddafi