walevi wa mistari waacheni wapepesuke | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

walevi wa mistari waacheni wapepesuke

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Davesto, Mar 1, 2012.

 1. Davesto

  Davesto JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 60
  kama mwaka unavyoanza na januari,
  nawaza mistari najaza daftari naanza safari,
  februari inanikuta kati ya bahari,
  vilindi vya maji mawimbi upepo kwa manuari,
  sigara mdomoni mfukoni najisachi,
  natoa kibiriti namoka naiota machi, akiba inasoma dola zaidi ya elfu mbili,
  haina noma naibana ili inifikishe aprili,
  kama sikosei uelekeo sipotei,
  nyakati zinasogea kuzinguka niko mei,
  nashika kanuni hisia fikra na dhumuni,
  nabuni michongo ubongo unawaza kufika juni, kama mbuni tuna mbawa ila hatupai,
  wanasema hatufai vipi tutaishi kuona julai,
  naota niko posti sina manoti nimeshalosti,
  naambiwa nitaachwa huru itapofika agosti,
  najihisi kama langa junki the ex-member,
  najipanga nauona mwanga wa septemba, ramadhani nafunga sunnah nifanya toba,
  nikingoja misosi iddi mosi oktoba,
  usawa butu pesa inaniacha solemba,
  ila bado nathubutu mpaka niibusu novemba,
  mi ni mwarabu mwenzao japo sina kilemba,
  asante mungu ndoto inakwisha mwisho wa desemba.....!
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  We broda unapoteza hela tu huku JF,...Nenda kachane mashairi uwe kama Dully!
   
 3. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Teh safi sanasana..una kipaji cha utunzi
   
Loading...