Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,677
- 22,946
Huko tuelekeako kuna dalili za kuzaliwa upya kwa jiji la Dar-es-Salaam na kuwa jiji linalostahiki hadhi yake kwamba ni jiji la maraha na linaloheshimika katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.
Dar-es-Salaam au mbingu ya Amani (heaven of peace) limekuwa ni jiji pana, na sehemu kubwa halijajengwa kwa mpangilio kiasi cha kuvuruga mipango miji ya kulifanya liwe jiji kamili lenye hadhi yake.
Kwa mujibu wa sensa ilofanywa mwaka 2012 jiji hili lina wakazi wapatao milioni 4,364,541 na ni jiji linaloongoza kwa kuwa na makazi yaso rasmi au "slams".
Makazi haya ni yale yaso na maji na huduma muhimu za msingi kama barabara, uzoaji taka na huku nyumba nyingi zikiwa zimejengwa bila mpangailio maalum.
Ni wazi kabisa kwamba ujenzi wa barabara za TAZARA, na miundumbinu mingine itawezesha kuwaondoa wafanyabisahara ndogondogo ambao wamekuwa wakiuza bidhaa zao pembezoni mwa barabara nyingi za jiji hili, katika maegesho ya magari na katika vituo vikuu vya mabasi.
Lakini mwendo wa serikali ya awamu ya tano katika kuboresha mazingira na ustawi wa jiji la Dar-es-Salaam kuna dalili kwamba wale wakazi ambao hawana ajira rasmi, hawalipi kodi na wanaishi kiujanjaujanja na wanaojishughulisha na biashara haramu za viroba na madawa ya kulevya, siku zao zinahesabika na itabidi waanze kurejea vijijini au mikoani walikotoka.
Litakuwa ni jambo la busara kwa wananchi ambao hawaja ajira rasmi wakafikiria kurejea vijijini ambako wanaweza kuanzisha miradi kadhaa ya kilimo ambao ndiyo uti wa mgongo wa taifa letu, badala ya kuendelea kuishi Dar-es-Salaam ambako wanaishi maisha ya kubahatisha.
Ule msemo wa kudai watu wanakwenda Dar-es-Salaam kutafuta maisha unakaribia kuzikwa rasmi.
Ukitaka kuishi Dar-es-Salaam basi utapaswa kuwa na ajira rasmi, unalipa kodi stahiki, na kama unafanya biashara basi iwe imesajiliwa kule BRELA na una namba ya kulipa kodi au TIN.
Hali hii itaenda sambamba na ujenzi wa mpangilio wa jiji na wale watanzania wenye uwezo wa kifedha kujenga nyumba bora na za maana na hata wale wenye ajira rasmi na walipa kodi wote kuweza kupata viwanja vya maana kuweza kujenga nyumba, hoteli, migahawa na miundombinu mingine ya maana.
Halikdhalika , wale watanzania wahandisi watapata fursa ya kuonyesha umahiri wao katika kuchora na kubuni ujenzi wa nyumba, maghorofa na miundombinu mbalimbali ili kazi zao zionekane rasmi na jiji la Dar-es-Salaam lipendeze.
Kwa kuwa Dodoma sasa ndiyo makao makuu ya nchi, basi hali hiyo imetoa fursa kwa serikali kujaribu kuliboresha jiji la Dar-es-Salaa ili liwe na hadhi yake inayostahili.
Je wewe unafikiriaje?
Tuepuke jazba tujenge hoja.