Baba ni baba tu hawezi kuitwa mnoko.
Baba yangu hakuwa na tabia ya kupiga piga ovyo na sijawahi kusikia tusi kinywani make, sijawahi kumuona anakunywa pombe wala kuvuta sigara, ni mtu wa dini sana kila ikifika siku ya ibada yupo na shughuli nyingi kama vikao kabla havijaanza anamtanguliza kwanza mungu.
Ila bado nilipofanya ujinga ujinga alinitandika vizuri, anaweza kusema baba kawahi kunipiga Mara saba tu toka nizaliwe, ila bado hofu ya baba ipo pale pale.
Kanisomesha shule ya msingi English medium, sekondari shule nzuri na chuo sikuwa na mkopo ila aliweza kunipa laki 3 kila mwezi haikuwa baba.
Pamoja na yote hayo, hofu ya baba ipo pale pale, kuongeleshana hivi siwezi labda yeye ndio aniite kuniambia au kunishauri jambo Fulani, na ushauri wake pamoja na maneno yake kwangu vina uzito sana.
Ila yote kwa yote mama ndio namuona kama besti tu, nakumbuka zamani hata nikichelewa kurudi nyumbani nlikuwa namfahamisha kwanza maza nikifika home anitetee kwa mzee.
Baba ni baba tu,