bryan2
JF-Expert Member
- Jun 8, 2016
- 3,321
- 4,671
Hii ilikua Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania,kulikua na mambo mengi Soka,kikapu,pete,kurusha Kisahani,Tufe,kukimbia,kwaya,hesabu klabu,lugha klabu...nk,ilikua burudani kwa kweli kuanzia ngazi ya Shule mpaka Taifa.
Nlifanikiwa kushirik michezo hii vipengele vya kwaya,michezo ya kiingereza/English drama na Dictation kwa wale walishiri watajua nlikua darasa la ngapi hasa hapo kwa Dictation,Kambi yetu ilikua shule ya Msingi Naura pale Arusha michezo ikifanyika viwanja vya Soweto na Amri Abeid Karume.
Kama kawaida siku za ufunguzi kulikua na shamrashamra sana tukiimba wimbo maalumu wa Umitamshumta na gwaride la nguvu,Penye wengi pana mengi kama kawaida vituko havikosekani kwa matukio kama haya.
Kwanza Ugeni wa mji hapo umetoka kijiji hata lami hujawai kuona kushangaa hapa na pale kwa Sana.
Utani baina ya wanafunzi,kupata marafiki wapya na kuanza kuandikiana barua baada ya kurudi enzi hizo hakuna cha wasaps wala twiter ni mwendo wa kwako mpenzi dhumuni la barua hii...
Baadhi ya timu za shule kupigwa goli nyingi sana,baadhi ya shule kuchezesha mamluki,kusogezeana vitu,etc
Tukumbushe na wewe changamoto/vituko ulivyokutana navyo katika michezo ya Umitashumta.