Tajiri wa Magomeni
JF-Expert Member
- Aug 21, 2019
- 4,274
- 2,921
ilikuwa mwaka gani?Nimetoka Dar nimeahidiwa tumiwa nauli, nikazama Darlux la Arusha nikamwambia Konda mpaka Chalinze nauli fresh!
Kibaha hola, naanza tetemeka, sina vocha sina kitu, wala message, aliyeahidi kimya, nikashushwa chalinze, nikatafuta mahali nikakaa!
Nimekaa mpaka saa 12 sijawa, sijanywa sina Vocha’s sina kitu, akatokea Mzee akanambia Kijana Nimekuona toka asubuhi shida nini?
Nikamweleza, akanambia chukua bag twende, kudadadeki, kanipeleka Guest kalipa 25,000/- nikaanza ogopa, akanipa cash 40,000/- akanambia Safari njema kesho!
Kaondoka, nikasema hapa yaweza kuwa msala siamini amini, cha kwanza nikahama Chumba, cha pili nikaenda tafuta chakula!
Sikuwahi mwona tena yule Mzee mpaka Leo wala hakurudi!