Pyepyepye
JF-Expert Member
- Jan 6, 2017
- 1,940
- 3,858
Habari ya jioni wanajamvi?
Wale tuliokwisha kupumzika tayari, poleni kwa majukumu ya wakutwa nzima, wale ambao tungali bado na mihangaiko na mizunguko ya hapa na pale pia poleni na hongera kwa kuendeleza maelekezo na maagizo tuliyopewa baada ya kuisikia sauti ya mwanamke badala ya sauti ya MUNGU yaani kula kwa jasho.
Leo napenda tushirikiane kwenye jambo hili kwa namna ya kupeana uzoefu lakini pia namna ya kujikinga na ajali ambazo kimsingi zinaweza kuepukika, uzoefu huu hasa kwangu mimi binafsi nategemea kuupata toka kwa madereva, watu wenye kusafir mara kwa mara, na hata mara moja moja na wamiliki wa vyombo vya moto kupitia michango zao watakazo ziweka hapa.
Kwa uzoefu wangu, nikiwa na miongo kadhaa juu ya uso wa dunia, sikuwahi kupata ajali kubwa zaidi ya kuanguka na baiskeli, mpaka mwaka 2015 mwezi wa 4 nikiwa na jamaa yangu tukitokea eneo moja linaitwa Makere lililoko wailaya ya Kasulu mkoani Kigoma, safari yetu hii ilikusudiwa kutufikisha nchi jirani ya Burundi kwenye eneo moja linaloitwa Susumo ikiwa ni sehemu ya kusaka maisha.
Tulianza safari mida ya saa 4 hivi, tukitumia usafiri wa pikipiki tulipita kambini (pale makere kuna kambi ya wakambizi) kwenye mida fulani ya mchana tulikuwa tukivuka eneo moja linaitwa Herubushingo, eneo hili linavilima fulani, ambavyo ikiwa ni mgeni utatakiwa kuwa na tahadhari kubwa, kwa sababu ya ugeni wa mvua na kipingi hiki ndo mvua zilikuwa zinaishiria, hatukujua kuwa njia imechimbika, ile tunakimaliza kilima tu, tuikuta na mteremko mkali, lakini kibaya zaidi ni kuwa barabara ilikuwa imechimbwa na maji kufuata, tairi za magari yanamopita, mimi na jamaa angu tukaingia kwenye ile mifereji na wakati huu tulikuwa na mwendo wa kawaida tu, hazikupita hata dakika mbili, tulijikuta tukiwa chini.
Jambo la kumshukuru MUNGU ni kuwa, mbali na kupasuka kwa maeneo kadhaa ya miili yetu, ikiwemo mimi pia kupasuka mdomo, hatukuumia sana. tulijizoa zoa hapo na kuanza kuikokota pikipiki yetu ambayo ilikuwa imeharibika sana, tulitembea kwa umbali mrefu bila kukutana na watu, lakini pia tulitembea kuanzia muda huo tuliopata ajali ambao naeza sema ilikuwa kama saa 8 hivi mpaka saa 11, ndipo tukafika kijiji ambacho tulipata huduma kadhaa kwa majeraha yetu lakini pia ikiwemo kutengenezwa kwa pikipiki yetu. Tulilala kwa mwenyekiti na kesho yake mchana tuliendelea na safari yetu hadi Susumo.
Jambo ambalo nimekuwa nikijiuliza ikiwa tulitembea kwa muda mrefu bila kupata huduma, vipi kama mmoja wetu angekuwa kajeruhika sana kiasi cha kutaka huduma ya haraka, je asingekufa?
Yote kwa yote namshukuru MUNGU kwani alitunusuru kwa janga kubwa tukiwa kwenye nchi ya ugeni.
Kwa wale wenye uzoefu na changamoto hii na nyingine nyingi za kujikuta ukihitaji msaada serious ilhali mazingira hayarusu na wala hayatoi mwanya wa msaada wowote, ebu tupeane uzoefu ikiwemo pia kulitukuza jina kuu la MUNGU kwa kututunusuru, dhidi ya kifo na kwa wakati ule.