Wale mlio kwenye mahusiano na watu wa namna hii, huwa mnayafurahia maisha?

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,511
40,609
Maisha yamekuwa na changamoto nyingi katika utafutaji, na kupelekea baadhi ya watu kutumia njia wanazo zijua wao ili waweze kufanikiwa.

Wapo walioingia maagano ya kumiliki vitu fulani ili maisha yao yaweze kuwa na mafanikio; mfano, wapo wale wanaovaa mapete makubwa, wengine kuna vitu wanaweka kwenye magari, majengo, nguo wanazovaa n.k, wengine wamechanwa miili yao na kupandikizwa vitu n.k

Na wengine baada ya muda fulani wanatakiwa wafanye ibada ili kudumisha yale maagano aliyopewa.

Sasa najiuliza; wale mlio kwenye mahusiano na watu wa namna hii, huwa mnayafurahia maisha?​
 
Aloelewa anieleweshe
 
Wwn unafikiria kuna mtu atakuja kusema uhalisia wa mambo hapa!??

Wengi wao utasikia niliwahi kua na mtu aliyekua hivyo kumbe ndio ako anaexperience wakati huu, ama atatoa ushuhuda kwa kumsemea mtu mwingine, ila sio rahisi kufunguka!!

Ww ungeuliza tu moja kwa moja kusudio lako nafikiri ingefaaa sana!
 
Najua kufunguka ni ngumu, ila wanaonekana, wanasema ni lazima ubebe msalaba uliouchagua.
 
Huwa wanaanzaga mbali kukuvuta taratibu kwa masharti rahisi mfano lete kuku lete ng'ombe kifuatacho mtu,ukinogewa wanakupumbaza utoki unakuwa mtumwa wao,kisha wanakudrive watakavyo wao ukitoka unakufa
 
Ukiwa na tamaa, unakuwa mtumwa, na maisha yako yanakuwa hayana furaha; ingawa wanaokutazama kwa nje wanakuona uko vizuri.
 
Wa
Ukiwa na tamaa, unakuwa mtumwa, na maisha yako yanakuwa hayana furaha; ingawa wanaokutazama kwa nje wanakuona uko vizuri.
Wafanyakazi wako ndio wanaofurahia utajiri wako, kama mshumaa na mwanga. Uoni madada na makaka wa Kazi wa matajiri walivyo na nuru kuliko matajiri wenye nyumba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…