Wale funza wa miguu waliishia wapi?

Wale funza wa miguu waliishia wapi?

Braza Kede

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Posts
5,165
Reaction score
8,959
Kwa faida ya wote hasa vijana wa kileo ni hivi hapo zamani sehemu kubwa za miji mingi haikuwa na lami.

Barabara nyingi zilikuwa ni za vumbi. Sasa hawa funza walikuwa ni wadudu wadogo mithiri ya viroboto wanaokaa kuzunguka sehemu ya jicho la kuku hawa wakijificha ndani ya hilo vumbi la barabarani. Wewe ukipita tu hapo basi tayari unao!

Funza aliingia kidoleni pale sehemu ya chini au juu ya ukucha na kuweka himaya yake hapo. Usipomtoa anataga mayai yasiyo idadi na kuzaliana hapo.

Ukichelewa zaidi kumtoa yale mazalia yanaenea maeneo mengine ya mguu. Usipokaa sawa mguu unapinda kuelekea upande mmoja yani kama ni wa kulia utapinda kuelekea kulia na kama ni wa kushoto utaelekea kushoto. bdae unaweza ukashindwa kabisa kutembea.

Hawa funza walikuingia kama umepita sehemu yenye vumbi hasa vumbi lile laini sana bila kuvaa viatu vya kufunika. Yaani ukivaa ndala, sendo, kobazi lazma uondoke nao. Leo hii ukimuona mhenga aliyepinda miguu kuna uwezekano mkubwa alipitiwa na funza miaka hiyoo!

Leo hii kwa maeneo mengi funza wamebaki kuwa ni hadithi ya kale kwani walitokomea wenyewe tu. Hadi sasa hakujawa na maelezo rasmi ya nini kilichosababisha funza kutokomea.
 
Braza Kede mara ya mwisho lini kufika Kigoma? Maeneo ya Manyovu, uvinza, Kakonko Nyakanazi n.k
Huko bado funza wametia kambi
 
Kwa faida ya wote hasa vijana wa kileo ni hivi hapo zamani sehemu kubwa za miji mingi haikuwa na lami.

Barabara nyingi zilikuwa ni za vumbi. Sasa hawa funza walikuwa ni wadudu wadogo mithiri ya viroboto wanaokaa kuzunguka sehemu ya jicho la kuku hawa wakijificha ndani ya hilo vumbi la barabarani. Wewe ukipita tu hapo basi tayari unao!

Funza aliingia kidoleni pale sehemu ya chini au juu ya ukucha na kuweka himaya yake hapo. Usipomtoa anataga mayai yasiyo idadi na kuzaliana hapo.

Ukichelewa zaidi kumtoa yale mazalia yanaenea maeneo mengine ya mguu. Usipokaa sawa mguu unapinda kuelekea upande mmoja yani kama ni wa kulia utapinda kuelekea kulia na kama ni wa kushoto utaelekea kushoto. bdae unaweza ukashindwa kabisa kutembea.

Hawa funza walikuingia kama umepita sehemu yenye vumbi hasa vumbi lile laini sana bila kuvaa viatu vya kufunika. Yaani ukivaa ndala, sendo, kobazi lazma uondoke nao. Leo hii ukimuona mhenga aliyepinda miguu kuna uwezekano mkubwa alipitiwa na funza miaka hiyoo!

Leo hii kwa maeneo mengi funza wamebaki kuwa ni hadithi ya kale kwani walitokomea wenyewe tu. Hadi sasa hakujawa na maelezo rasmi ya nini kilichosababisha funza kutokomea.
Bado Kuna watu wana funza huko vijijini ndanindani
 
Matumizi ya maji na sabuni yamechangia sana kupungua kwa funza ingawa bado wapo sehemu zilizosahauliwa, zisizo na lami. Funza chawa na kunguni ni kielelezo cha uchafu wa mwili na kutokujali kanuni za afya.
 
Back
Top Bottom