Wakware someni hii!

MTAZAMO

Platinum Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
20,209
Reaction score
35,852
Nilikuwa nimekaa na dada mmoja mahali kwenye public ghafla yule dada akapigiwa simu na kupitia mazungumzo yao inaonesha hawafahamiani.

Yule dada akauliza umenijuaje na umepataje namba yangu,baadae yule dada nikasikia akikiri kufanya kazi sehemu flani na inaonesha jamaa alipata hiyo namba hapo ofisini baada ya kufurahishwa na huduma(kwa mujibu wa mazungumzo yao)

Baadae yule dada akamwambia mpiga simu yule awe na subira maana yupo sehemu ya public hawezi kuongea kwa uhuru.

Baada ya simu kukatwa immediately yule dada kampigia rafiki yake anayefanya kazi kwenye moja ya mitandao ya simu na kumtajia ile namba aliyopigiwa na kuomba yafuatayo:-

1) Jina la mwenye namba
2) alipo muda huo
3) umri wake
4) kabila lake
5) anapoishi
6) amejiandikisha kwa kitambulisho gani

Baadhi ya hayo maswali nilisikia wakizungumzia na yule mkware.mfano binti alimuuliza jamaa alipo muda huo!

Hazikupita dk 5 dada akapewa details zote! na akamwambia shoga yake kuna mtu hamjui anamtongoza hivyo alitaka kuwa na taarifa zake mapema.

Wakware kazi kwenu binti atakuwa anamchora tu huyo jamaa.
 
hiyo ndo habari ya mujini.....
 
Na wenye simu zilizosajiliwa kwa jina la kampuni?
 
Yaani the way yule binti alivyokusanya data haraka nilichoka kabisa! binti mwenyewe yupo kwenye late twenties hivi hivyo kujua umri sahihi wa jamaa itamsaidia kujua kama ni saizi yake ama!
 
.....aaahh,huyo dada anafaa kuajirwa na wala hafai kibiashara!sio risk taker!
 
operators wa siku hizi wanamisconduct kazi hamna confidentiality kabisa yaani.
 
OOOPPS! Nilidhania ni WAKWERE tuwajuao...Maana yao ki ukweli yanatosha bila sub-sector
 
Hujakosea Tetra ni kweli kabisa "New generation at work" Short and clear huhitaji kuumiza kichwa
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…