Wakuu Wa Rais Kiutawala

Wakuu Wa Rais Kiutawala

fingwele

Member
Joined
Oct 7, 2018
Posts
26
Reaction score
13
Habari wana JF. Kumetokea maneno mengi mitandaoni kuhushu msimamo wa Rais kuhusu katiba mpya na kuwalaumu sana washauri wake wakiwemo mawaziri haswaa Waziri Kabudi. Kwa maoni yangu kama raia huru ni kwamba:- Rais wa nchi yetu kiutawala hutenda kazi zake kwa kuongozwa na katiba ya nchi ambayo kwayo yeye amepatikana na kuongozwa na sheria za nchi na kanuni zake baada ya mkutano wa wananchi yaani Bunge kutunga na yeye kupitisha kwa madai ya katiba aliyopatikana kwayo. Hivyo hadi hapo Katiba ya nchi na Sheria zake ndizo naweza kusema kuwa ni wakuu wa Rais katika kufanya kazi zake za utawala wa nchi yetu na sio maelekezo yo yote toka kwa mtu yo yote maana hakuna mwenye mamlaka zaidi yake katika uongozi wa nchi. Hivyo, Nje ya katiba na Sheria, kiutawala hakuna mtu mwenye mamlaka ya kutoa maelekezo kwa Rais ili ayafanyie kazi bali watu wanaweza kumwomba au kumshauri Rais kufanya jambo fulani na yeye mwenyewe kwa mapenzi yake na wema wa uongozi wake kwa nchi akiona inafaa kufanya hivyo anaweza kufanya. Hivyo kuwalaumu mawaziri au washauri wa Rais ni kuwatendea isivyowastahili kwakuwa hao hutenda kazi zao kikatiba na kisheria pamoja na kutekeleza maelekezo ya Rais ambaye ndiye aliyewachagua wawe wasaidizi wake kwa kazi za kuliongoza Taifa. Kwa Rais kukataa hitaji la katiba mpya kwa sasa nadhani anaamini kwamba katiba iliyomuweka kwenye Urais wa nchi yetu bado inamsaidia kuiongoza nchi kiutawala na namna ya kuwaelekeza wasaidizi wake kufikia lengo la kuwaongoza wananchi. Labda kwa ambao hatujapendezwa na msimamo wa Rais kuhusu katiba mpya kuwa sio kipaumbele chake kwa sasa, tunayo nafasi kwa uchaguzi ujao kuwaona wagombea Urais wa vyama vya upinzani na CCM watakaokuja na kipaumbele cha katiba mpya na ikiwa watafaa kwa tabia, uwezo na elimu zao kuiongoza nchi tuwachague na kura zao zikitosha kumzidi Rais wa sasa basi watatuletea katiba mpya.
 
Back
Top Bottom