Wakuu wa mikoa mingine nyie mnatusaidiaje wanawake wa mikoa tofauti na Dar?

Dejane

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
49,659
68,625
Jana tumeshuhudia kina mama wengi waliotelekezwa na watoto wakiwa kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar Mh. Makonda, ni jambo zuri lakini nadhani si zuri kivile maana sijajua kajipangaje ili uwe mpango wa kudumu ikiwezekana kina mama wasihangaike tena au kulalamika kuhusu kutelekezwa na kina baba.

Mimi nadhani hilo swala lisingekuwa la Dar peke yake tulifanye la Tanzania nzima, maana navyojua kuna wizara husika inahusika na hili na wala hawafatilii.

Kwanini Makonda asingejipanga hilo swala likajadiliwa upya bungeni na wizara husika ili kupanga mipango madhubuti ya kuwadhibiti wanaume/waume wanaokimbia familia zao au wanaozalisha hovyo hovyo, ikawekwa sheria kali ili mtoto apate haki zake za msingi na sio kutafuta kiki kwa muda mfupi inakuwa kama haijatusaidia wanawake.

Tunaomba wizara husika iangalie hili swala na sheria ziwe kali ili watoto watunzwe na wapangiwe kiasi cha kutoa kwa mwezi, sheria zibadilishwe maana hali ya maisha imezidi kuwa juu maisha yamekuwa magumu na wahitaji ni wanawake wa Tanzania nzima sio Dar tu tunaomba tueleweke kwa hili.

Serikali pia tunaomba iongeze somo la ziada na semina mbali mbali za kuwaelimisha watoto wa kike wajue wanatakiwa umri gani wawe na watoto, matumizi ya condom ikiwezekana watoto wanapovunja ungo waanze kugawiwa condom maana hata tusipowapa wanafanya wafundishwe mapema na kujiepusha na mapenzi katika umri mdogo basi wakizidiwa watumie zana, ili kujiepusha na magonjwa na mimba zisizotarajiwa.

Tukatae tukubali watoto wanafanya mapenzi wakienda tuition, shuleni, tukubali tu watumie condom tukiwaelewesha nadhani itasaidia ili tupunguze watoto wa sio na walezi wengi najua wengine mtaponda ila ukweli ndio hivyo hali ni mbaya mitaani kwenye jamii zetu watoto wengine sana mimba wakiwa wadogo unadhani watafanyaje mtoto anazaa mtoto mwenzie bora waelimishwe au kuna njia nyingi za kuzia mimba zifanywe kila mzazi atambue hilo tukiwaachia ni mimba tu .


Wanaume na nyie tumieni Condom mbona hamna huruma kabisa mnatembea na vitoto vidogo kama watoto wenu kwa kuvilaghai kutokana na umaskini wanaume Hamna huruma na upendo kabisa baadhi yenu, mkiwapa mimba watunzeni mpaka muitwe na Mkuu Mkoa jamani.

Wakuu wa mikoa mnahangaika kweli mwingine kaita wanawake, mwingine kaenda fundisha shuleni kazi ipo mwaka huu.

Bila kusahau na nyie wanawake msirubunike na msipende kutumiwa kwa muda mfupi.
 
Nimekuelewa, wanawake wawe chachu ya mabadiliko, wajue impact ya kufanya mapenzi kabla ya muda na bila ya kinga, pia wanaume waache ufala unalalaje na mwanamke na kumpa mimba wakati unajua aidha una familia au hutotunza mimba na mtoto? Hali ya jana inaonyesha dhahiri kuwa condom hazitumiki ipasavyo watu wanajilipua tu ndo matokeo ya kupata mtoto usiyemtarajia
 
Nina amini kuwa asilimia kubwa ya wale wanawake waliokwenda Jana kwa Prince hawawajui waliowazalisha labda yule mchina was Ng'ong'ona...
 
Starehe mzitake halafu kazi ya kutafuta mahawara zenu wafanye wengine! ebo! hayo atafanya makonda tu. Ma- RC wengine wana kazi muhimu za ujenzi we taifa. pambaf zenu na starehe zenu!
 
Dinazarde
Halichofanya Makonda kuitisha maandamano au Tangazo la udhaifu wa sheria nchini nina maana serikali na bunge lilichukue litungie sheria mpya na zitakazo tumika nchi nzima .lakini kwa ccm ilivyo hiyo ni advantage ya kujipatia ujiko sii ajabu kila mkoa ukafuatisha kwa staili hiyo hiyo ya maujiko na kwa maana hiyo unaweza subiri tuu watalianzisha na hapo mkoa kwako
 
Nimekuelewa, wanawake wawe chachu ya mabadiliko, wajue impact ya kufanya mapenzi kabla ya muda na bila ya kinga, pia wanaume waache ufala unalalaje na mwanamke na kumpa mimba wakati unajua aidha una familia au hutotunza mimba na mtoto? Hali ya jana inaonyesha dhahiri kuwa condom hazitumiki ipasavyo watu wanajilipua tu ndo matokeo ya kupata mtoto usiyemtarajia
wote iwe jukumu letu kila mtu ahakikishe mwenzie hapati mimba na hampi mtu mimba
 
nikusomeje? Wewe unataka kila aanzishapo kitu huyu nyumbu watu wote wafuate? Vipo vya kufuata lakini sio huo upuzi, umejiuliza gharama analipa nani?
sio wafatishe ndio maana nikaelezea hili tatizo ni Tanzania nzima
 
Ni uzwazwa tu wanawake kutokuwa na taarifa au elimu juu za haki zao pindi wanapolekezwa, KWANI USTWI WA JAMII SI PAPO!! KWANINI HAWAENDI KUPATA MSAADA WAKISHERIA?
 
Back
Top Bottom