Wakuu wa majeshi ya ulinzi na usalama

McCain

JF-Expert Member
Dec 2, 2016
1,169
517
Jamani kwann wakuu wa majeshi ya ulinzi na usalama mara nyingi wanatokea JWT na sio majeshi mengine kama polisi, magereza, uhamiaji, jkt nk
 
Swali nyeti sana hili.

Ila wengi nasikia wanatoka kule Military Intelligence kwa hiyo hata huko JWTZ na JKT sio kila mtu ana nafasi ya kuwa Mkuu wa Majeshi.

Ni wazee wa kitengo nyeti tu ndio wanakamatia hio ofisi.
 
Mwamnyange na Mabeho walikuwa JKT, unajua hilo? Police kazi yake ni kudeal na raia, Magereza wafungwa, Uhamiaji kudeal na wanaotoka na kuingia Tanzania kihalali. Sasa wazee wenyewe ambao ni JWTZ na kitengo chake cha kutafuta aka JKT wao ndiyo wenye jukumu la kulinda mipaka ya nchi ya Ardhini, majini, na angani. Logic inakupa kuwa hawa ndiyo haswa wenye jukumu la ulinzi. Hapo ujue karibia 3/7 ya TISS ni JWTZ.
 
Mwamunyange unajua alitokea wapi?

SWALI LA KITOTO HILO RUDI DARASANI UKIJUA MAJUKUMU YA MAJESHI ULIYOYATAJA PIA UTAJUA KWA NINI JWTZ WANAONGOZWA NA MWANAJESHI ANAYEJUA VITA HAO WENGINE HAWAJA SPECIALISE KWENYE VITA WENGI WAMESOMA SHERIA NA HAKI ZA KIJO BISIMBA
 
Kukujibu swali lako kwanza hakuna mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama

Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama ni rais tu ambae ndie amiri jeshi mkuu wengine wote ni wakuu wa jeshi na ndani ya jeshi kuna vikosi mfano

Kuna mkuu wa Jeshi la ulinzi (JWTZ)
ndani ya Jeshi la Ulinzi kuna vikosi ambavyo ni
JKT na ndani ya jeshi kuna kamandi ambazo zinakuwa na wakuu wake ambazo ni
1 Anga
2maji
3 Aridhini
Ambavyo vyote vinakuwa na wakuu wake ambao wote wanareport kwa mkuu wa Majeshi ya Ulinzi

Pia kuna mkuu wa vikosi vya usalama ambaye ni IGP (POLICE TZ) ndani ya Police kuna vikosi na ambavyo vinawakuu wake

1 Jeshi la magereza
2Jeshi la zimamoto
3 Kikosi cha kutuliza ghasia FFU
4 Uhamiaji

Vikosi vyote vinakuwa na mabosi wao lakini wote wanareport kwa IGP kama mkuu wa jeshi la Police TZ

Kumekuwa na tatizo la kuchanganya majina hasa kwa Tanzania neno Jeshi lingetumika kwa jeshi tu duniani unaposikia army unajua ni watu gani Police wangebaki na vikosi au kikosi cha usalama au Police tu si wao kujiita jeshi

TISS si jeshi au kikosi aidha cha Ulinzi ( protection) au Usalama ( security) ukizungumzia Ulinzi unamaana ya JESHI ukizungumzia Usalama inamaana ya POLICE

Unapozungumzia TISS unazungumzia (Intelligence) na unapozungumzia INTELLIGENCE unazungumzia mchanganyiko wa( Protection +security ) yani Ulinzi na Usalama vyote kwa pamoja ndani ya taasisi moja so TISS ni taasisi na taasisi inaweza kufanya kazi sehemu yeyote lakini jeshi au police hawawezi kufanya kazi sehemu yeyote
Ndio maana unaweza kuwakuta TISS wako Police,Jeshini ,Mitaani ,Wizarani na sehemu nyingine zote kwa maana ni Taasisi si Jeshi au Kikosi

McCain kirikou1
 
Jeshi=Army
Ni kiswahili pekee ndo upelekea kuwa katika kundi moja mfano jeshi la polisi,jeshi la magereza lakini inreality polisi siyo jeshi wala magereza sio jeshi.
Jeshi( ARMY) ni JWTZ,JKT.
polisi ni TPF - Tanzania police force
 
Magereza Police Uhamiaji Mafunzo yao Ni TOFAUTI Na JWTZ

Hao JWTZ Mafunzo yao Wanadili Na Usalama Wa Nchi Kwa Ujumla
 
Swali nyeti sana hili.

Ila wengi nasikia wanatoka kule Military Intelligence kwa hiyo hata huko JWTZ na JKT sio kila mtu ana nafasi ya kuwa Mkuu wa Majeshi.

Ni wazee wa kitengo nyeti tu ndio wanakamatia hio ofisi.
Inamaa jeshi la policcm haitatokea hata ndoto
 
SWALI LA KITOTO HILO RUDI DARASANI UKIJUA MAJUKUMU YA MAJESHI ULIYOYATAJA PIA UTAJUA KWA NINI JWTZ WANAONGOZWA NA MWANAJESHI ANAYEJUA VITA HAO WENGINE HAWAJA SPECIALISE KWENYE VITA WENGI WAMESOMA SHERIA NA HAKI ZA KIJO BISIMBA
Sikila anayeuliza ni mjinga wengine wanataka kujiridhisha kwa kile wanachokijua kuwa ni sahh hata wewe unaweza kujifanya unajua kumbe unachokijua sio sahh
 
Back
Top Bottom