Wakuu ukame umeanza kunifilisi

Mtu mdogo

JF-Expert Member
Nov 2, 2016
525
826
Mimi ni kijana wa makamo ambae nilianza kujishughurisha na ufugaji wa mbuzi na ng'ombe kwa muda mrefu tokea nikiwa chuo kikuu

Nilianza ufugaji baada ya kupata pesa ya kujikimu nikawa natuma kijijini wananunua mifugo hivo badae nikajikuta nina ng'ombe na mbuzi wengi katika ranchi yangu

Ila mimi nipo dar es salaam kibiashara lakini ranchi yangu ipo ukerewe taarifa ninazo zipata hapa ni kuwa mnvua hamna kwa kipindi kirefu hivo majani yamekauka na malisho yamekuwa magumu na baadhi ya ng'ombe wameanza kudhoofu mbuzi wanakula majani ya mipapai ndo ipo kwa wingi

Inanilazimu kuanza kuuza kwa hasara ili kuokoa angalau fedha yangu kidogo

Inshort naona dalili za umasikini zikinijia

Tuombee mnvua jamani ije wengine tunaitegemea
 
Uza upesi, juzi Kuna ngo'mbe kafa hapa barabaran maenei ya Boma jaribu Na KIA, Yan pakame balaa, hamna hata jani
 
Wewe kama msomi wa chuo kikuu, ufugaji wako ulitofautiana vipi na wa mfugaji ambaye hajasoma? Japo risk assessment and mitigation plans. Lengo lako lilikuwa ufugaji wa kibiashara au prestige kuwa una idadi kubwa ya mifugo?
 
Hujui unachosema nimefuga kisomi kabisa wapo kwenye ranch wanalishwa kwa kukatiwa majani na nimefuga kibiashara nauzaga mafahari majike naacha ili yazaliane na kutoa huduma ya maziwa
 
Uza upesi, juzi Kuna ngo'mbe kafa hapa barabaran maenei ya Boma jaribu Na KIA, Yan pakame balaa, hamna hata jani

Asante mkuu ndo nimeanza kuwapunguza ningekuwa na uwezo ningewasafirisha kwenda maeneo rafiki
 
Cha msingi tufanyacho wenzio kipindi hiki cha ukame tunakusanya ngome waliodhoofu Kwa ukame Kwa bei ya kutupa tunapeleka Ranchi tunafanya kazi ya kusomba nyasi na pumba Kwa fuso tunasubiria mvua ikianza kunyesha mifugo inapanda bei tunauza Kwa bei kubwa cha msingi ukiweza kodi gari wasombee nyasi au uza ubaki na wachache.hio Pesa tunza hali ikiwa nzuri anza kufuga tena
 
Pole mkuu, ila hakuna mtu asiyetegeme mvua kwa namna moja au nyingine.Wengi tumeathirika sana.Ila afadhali wewe ambaye una an alternative means of survival.Wengine wanategemea either mifugo,crops or both.Hao hali yao ni mbaya sana.

Ila maombi peke yake hayatoshi mkuu,ni lazima tuache uovu wetu.Uovu umezidi sana. Mungu anaonyesha wazi sasa hasira zake kwetu.Ni wazi kwamba amemruhusu Shetani atushuhulikie.

Kama tusipotubia uovu wetu, we should expect an even worse scenario!
Mimi ni kijana wa makamo ambae nilianza kujishughurisha na ufugaji wa mbuzi na ng'ombe kwa muda mrefu tokea nikiwa chuo kikuu

Nilianza ufugaji baada ya kupata pesa ya kujikimu nikawa natuma kijijini wananunua mifugo hivo badae nikajikuta nina ng'ombe na mbuzi wengi katika ranchi yangu

Ila mimi nipo dar es salaam kibiashara lakini ranchi yangu ipo ukerewe taarifa ninazo zipata hapa ni kuwa mnvua hamna kwa kipindi kirefu hivo majani yamekauka na malisho yamekuwa magumu na baadhi ya ng'ombe wameanza kudhoofu mbuzi wanakula majani ya mipapai ndo ipo kwa wingi

Inanilazimu kuanza kuuza kwa hasara ili kuokoa angalau fedha yangu kidogo

Inshort naona dalili za umasikini zikinijia

Tuombee mnvua jamani ije wengine tunaitegemea
 
Hujui unachosema nimefuga kisomi kabisa wapo kwenye ranch wanalishwa kwa kukatiwa majani na nimefuga kibiashara nauzaga mafahari majike naacha ili yazaliane na kutoa huduma ya maziwa
Unajua maana ya ranch? Hiyo farm yako haijakidhi vigezo vya kuitwa ranch mkuu! Sema unafuga kienyeji yaani ng'ombe 100 wanakatiwa majani? Inakuwaje unaweka ng'ombe 100 Ukara? ARDHI haitoshi!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom